Mtazamo wa Uturuki kwa Mashariki ya Kati

Mtazamo wa Uturuki kwa Mashariki ya Kati

Mtazamo wa Uturuki kwa Mashariki ya Kati

LIBYA MPYA BAADA YA DAESH

Baada ya miezi 6 ya mapambano makuu dhidi ya DAESH hatimaye mji wa Sirte ni huru kutokana na vitisho vya wanamgambo wa DAESH .Wanamgambo wa DAESH walichukua udhibiti wa jiji la Sirte tangu mwaka 2015.DAESH walikuwa na urahisi wa nguvu katika eneo hilo kwa kuwa kulikuwa hamna mamlaka yoyote iliyokuwa inaongoza katika kanda hiyo.

Sasa Sirte ni hutu kutokana na vitisho vya mashambulizi ya magaidi hao,lakini bado kuna matatizo makuu ambayo sharti yatatuliwe.Changamoto hizi ni kutatua matatizo mengi ya kisiasa,usalama na kiuchumi.

 

Sirte ilikuwa miji muhimu kwa DAESH kando na Iraq na Syria ambapo wanamgambo hao walikuwa pia wamechukua udhibiti.Sirte ilikuwa na faida kwa DAESH hasa kwa kuwa ipo karibu na mipaka ya bara la Ulaya .Sirte ipo umbali wa kilomita 150 kutoka pwani ya bahari ya Mediterania .Hata hivyo ushirikaino baina ya jeshi la Misri na Taifa ya Maridhiano ya UMH inayopata msaada kutoka kwa UN ulizua matunda katika kupambana na DAESH katika kanda hiyo.

Serikali ya UMH ilikuwa na chagua moja tu la kuweza kuondoa DAESH kutoka Sirte hasa kuwa katika nchi ambyo ina serikali tatu tofauti.Pia UMH ılibidi kupambana na kuweza kuwashinda wanamgambo wa DAESH ili kuweza kupata msaada kutoka kwa jeshi la Misri.

 

Hilo ilikuwa mbinu moja pekee ambayo waziri mkuu wa UMH angetumia ili kuepukana na kutaka msaada kutoka serikali ya Marekani.Tangu Agosti moja ndege za kivita za Marekani zilianza kushambulia kambi za DAESH kutoka angani maeneo hayo.Hata hivyo raia wa Libya walionyesha mapambano kamili dhidi ya DAESH.Jeshi la UMH lilipoteza askari 730 katika mapambano hayo huku takriban 3,000 wakijeruhiwa.

 

Sasa swali kuu katika suala hili ni Je,msaada kutoka Marekani utaweza kurudisha Uadilifu wa  nchi ya Libya baada ya serikali ya UMH kufaulu ktika mbinu yake ya mapambano dhidi ya DAESH?

 

Kwa bahati mbaya jambo hilo halitakuwa rahisi.Kuna masuala makuu matatu ambayo yanafaa kutatuliwa kabla ya serikali yenye vyama kadhaa pinzani nchini kupewa mamlaka kamili nchini Libya .

 

Mojawapo ya masuala haya ni uwezekano wa DAESH kuleta vitisho tena katika kanda hiyo.

Bila shaka Sirte ni mojawapo ya malengo makuu na pia mikakati ya kundi la DAESH .Hii ni kwa sababu ya jiografia ya eneo hilo la Sirte .Hivyo basi haimanishi kuwa kushindwa mjini Sirte ni kushindwa katika maeneo yote mengine nchini Libya.Kwa kuwa ni desturi ya DAESH kupatikana katika maeneo mengine nchini Libya na pia hali ya anga ya jangwani pia inachangia pakubwa kwa uwezekano wao kurudi tena .Eneo hilo pia lina idadi chache ya watu na pia mipaka yake haina usalama imara jambo ambalo pia litapelekea kuwa na uwezekano wa wanamgambo hao kurudi tena .Vile vile pia kuna uwezekano Boko Haram na Al Qaeda kutoa misaada kwa kundi hilo .

Hivyo basi hatari na vitisho kutoka DAESH haiwezi kusemekana kuwa imemalizwa kabisa .

 

Suala lingine muhimu ni kuwa kushindwa kwa DAESH kwaweza sababisha mvutano zaidi baina ya UMH na vikosi pinzani katika eneo hilo .

Hasa kutoka upande wa vikosi vya jeshi la Libya la LMO linaloongozwa na jenerali Khalifa Hafter ambaye ameleta ushawishi mkuu kwa baraza la wawakilishi la Tobruk.Ushindi wa UMH mjini Sirte ni ishara na alama ya hadhi kuu  kwa serikali hiyo .Hata hivyo Hafter ana mipango ya kuzuia hadhi hii kuu kuonekana .Hii inaonekana hasa baada ya kuzuru Moscow ilikupata msaada kutoka Urusi na pia kutoa wito kwa wafuasi wa magharibi mwa Libya ili kuungana katika ‘Ukombozi wa Tripoli.’

 

Nalo suala la tatu ni mashindano kuhusu utawala wa ardhi hasa kwa ajili ya maeneo ya mafuta .

Rasilimali za mafuta ni miongoni mwa mambo muhimu katika nchi na pia utawala wan chi hiyo.Hii ni kwa sababu sekta inayotoa udhibiti wa sekta hiyo pia itaoongoza pato la nch na hivyo basi kuathiri ustawi wa nchi hivyo basi kuathiri pia ukuaji wan chi hiyo kwa ujumla .

 

Wakati ambapo UMH ilikuwa inapambana na DAESH,Hafter naye alionyesha dunia nzisma kuwa nalinda kanda ya mafuta ya Petroli ya Libya ya Crescent Petroleum hatua ambayo ilikuwa ya muhimu sana .Hatua hiyo ilikuwa ya kuondoa muonekano wa  juhudi ya UMH ya mapambano dhidi ya DAESH.Kwa kuchukua udhibiti wa eneo hilo la mafuta Hafter alikuwa na lengo la kuonyesha dunia kuwa serikali ya UMH haina mikakati ya kulinda  raslimali ya nchi .Pia inataka kuanzisha uuzaji wa mafuta nje ili kuimarisha uhalali wa umiliki wake .

 

Ushindi wa Libya dhidi ya ugaidi umedhihirisha kuwa Libya itaweza kufanikiwa zaidi ikiwa watafanya muungano dhidi ya aduai moja .Pili Libya yafaa kutambua kuwa migawanyo yao ya ndani ilisababisha DAESH kuweza kuingia ndani ya nchi.Hivyo basi sharti vita baina ya wapiganaji wa kijeshi wa ndai vimalizwa kwa haraka iwezekanavyo.

 

Pia jambo ambalo haliwezi pia kufichika ni kuwa migawanyiko na vita vya wenyewe kwa wenyewe pia vinashinikizwa na nguvu za kimataifa .Nguvu hizi za kimataifa kwa kawaida hazileti faida kwa raia wa Libya lakini pia jambo la kusikitisha ni kuwa haiwezeani kwa Libya kutatua matatizo yao wenyewe kwa sababu ya hali ya ghasia ya sasa .

 

 


Tagi: DAESH , UMH , Sirte

Habari Zinazohusiana