"Upinzani kushiriki katika mkutano Arusha kwa niaba ya Burundi"

Mpatanishi wa mzozo wa Burundi  atao wito kwa upinzani kushiriki katika mkutano Arusha Tanzania

"Upinzani kushiriki katika  mkutano Arusha kwa niaba ya Burundi"

 

Ofisi ya mpatanisha wa mzozo wa Burundi , rais wa zamani wa Tanzania Benjamin Mkapa ametolea wito upinzani kushiriki katika mkutano mjini Arusha.

Wito huo kwa wapinzani wa serikali ya Bujumbura waishio uhamishoni umetolewa  ili kuweza kupatia suluhu mzozo wa Burundi.

Mkutano huo unatarajiwa kufanyika ifikapo Januari 16 mjini Arusha kaskazini mwa Tanzania.

Dhumuni la mkutano huo ni kutathmini hatua na vizingiti katika kutafuta suluhu la mgogoro wa Burundi.

Ifahamike kuwa umoja wa CNARED ambao unakusanya vyama vya upinzani umempinga mpatanishi baada ya kusema kuwa rais Nkurunziza alikuwa na haki kuwania kiti cha urais kwa muhula wa 3.Habari Zinazohusiana