Magaidi 81 wa Al Shabab wauawa Somalia

Takriban magaidi 81 wa kundi la Al Shabab wameripotiwa kuuawa katika jimbo la Jilib nchini Somalia.

Magaidi 81 wa Al Shabab wauawa Somalia

Takriban magaidi 81 wa kundi la Al Shabab wameripotiwa kuuawa katika jimbo la Jilib nchini Somalia.

Waziri wa mawasiliano Abdurahman Osman ametangaza kuwa magaidi hao wameuawa katika operesheni mbili tofauti.

Waziri huyo amekiambia kituo cha habari cha SONNA kuwa jeshi la Somalia likishirikiana na nchi za nje zimetekeleza operesheni hiyo.

Ripoti zinaonyesha kuwa magari pamoja na silaha za magaidi hao zimeteketezwa katika operesheni hiyo.

Kundi la Al Shabab limetangaza kuhusika na Al Qaeda na imekuwa ikifanya harakati dhidi ya serikali ya Somalia toka liondolewe katika mji mkuu na Umoja wa Afrika mwaka 2011.

 

 Habari Zinazohusiana