Watu 30 wafariki katika ajali ya treni DR Congo

Watu 30 wafariki kıatika ajali ya treni iliotokea katika jimbo la Buyofwe Lualaba Kusini-mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo

Watu 30 wafariki katika ajali ya treni DR Congo

 

Watu 30 wameripotiwa kufariki na wengine kadhaa kujeruhiwa katika ajali yua treni iliotokea  mkoani Lualaba Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.

Watu zaidi ya 10 wamejeruhiwa katika ajali  kama alivyofahamisha  mkuu wa eneo la Lubudi Georges Kazadi.

Kiongozi huyo ak.ishirikiana na mamlaka ya reli hawakutoa taarifa yeyote kuhusu sababu zilizopelekea ajali hiyo.

 Treni hiyo iliofanya ajali ilikuwa ikiendesha usafirishaji wa bidhaa mahitaji kati ya jiji la Lubumbashi, Katanga na Luena Lualaba.Habari Zinazohusiana