Rais wa Burundi atuhumu baadhi ya mataifa ya Magharibi kusababisha soko la watumwa Libya

Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza alaani vikali kuuzwa kwa mnada wahamiaji walioshikiliwa nchini Libya

Rais wa Burundi atuhumu baadhi ya mataifa ya Magharibi kusababisha soko la watumwa Libya

 

Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza amelaani vikali kitendo cha kuuzwa kwa mnada  kama watumwa wahamiaji walioshikiliwa nchini Libya.

Libya kwa upande wake ilitangaza Jumapili kuwa  tayari imeanzisha uchunguzi.

Rais wa Burundi amejiunga na ulimwengu kukemea kitendo hicho katika ujumbe wake aliopeperusha katika ukurasa wake wa Twitter.

Katika ujumbe wake huo rais wa Burundi  ametuhumu baadhi ya mataifa ya Magharibi kushambulia Libya  kinyume na uamuzi wa Umoja wa Afrika.Habari Zinazohusiana