Fedha za wizi za rais wa zamani wa Nigeria kurejeshwa nchini Nigeria

kiasi cha dola milioni 321 za Marekani zilizoibiwa na rais wa zamani wa Nigeria Sani Abacha  kurejeshwa nchini Nigeria kutoka  Uswisi

Fedha za wizi za rais wa zamani wa Nigeria kurejeshwa nchini Nigeria

 

Shirika la kimataifa la kupambana na rushwa  lilimshutumu rais wa zamani wa Nigeria Sani Abacha kupora  kiwango hicho cha pesa na kuzihifadhi nchini Uswisi.

Sani Abacha aliongoza Nigeria kama rais mwaka 1993 hadi mwaka 1998.

Kwa kipindi  cha miaka  mitano Sani Abacha alijikusanyia utajiri  kinyume na sharia.

Mwaka 2014 familia ya Sani Abacha  ilikubaliana na serikali ya Nigeria kurejesha  kiwango cha pesa kilichoibiwa na kutoa sharti kufutiwa mashtaka yaliokuwa yakiikabili.

Serikali ya Uswisi, Nigeria na Benki ya Dunia  zimekubaliana kurejesha pesa hizo nchini Nigeria kuptia miradi ya maendeleo  itakayosimamiwa na  kuratibiwa na Benki ya Dunia.Habari Zinazohusiana