Zaidi ya raia 400 wa Nigeria warudishwa kutoka Libya

Takriban wanigeria 401 waliokuwa wamenaswa nchini Libya wamerudishwa nchini kwao ndani  ya masaa 24 yaliyopita.

Zaidi ya raia 400 wa Nigeria warudishwa kutoka Libya

Takriban wanigeria 401 waliokuwa wamenaswa nchini Libya wamerudishwa nchini kwao ndani  ya masaa 24 yaliyopita.

Kati ya waliorusishwa Nigeria 65 walikuwa ni wanawake,179 wanaume,watoto 7 na watoto wachanga 6.

Ripoti zinaonyesha kuwa watoto 4 kati ya 6 walikuwa wanahitaji huduma ya afya.

Hatua ya kurudishwa kwa raia hao ni baada ya habari kusambaa kuwa mamia ya wananchi kutoka nchi mbalimbali bara ni Afrika wamekuwa wakikamatwa na kuuzwa kama watumwa  nchini Libya.

Wengi wao wanasemekana kuwa ni waafrika waotaka kuvuka kuelekea Ulaya kupitia bahari ya Mediterranean .

Tagi: Libya , Nigeria

Habari Zinazohusiana