Museveni aweka wazi kutokuwa na nia ya kuachia madaraka

Rais wa Uganda Yoweri Museveni kwa mara nyingine ameweka wazi nia ya kukaa madarakani hata baada ya kuvuka umri wa miaka 75.

Museveni aweka wazi kutokuwa na nia ya kuachia madaraka

Rais wa Uganda Yoweri Museveni kwa mara nyingine ameweka wazi nia ya kukaa madarakani hata baada ya kuvuka umri wa miaka 75.

Katika mkutano uliofanyika Ikulu siku ya Jumatano,Museveni mwenye umri wa miaka 73 aliiambia kamati ya bunge kuwa mataifa mengi yaliyoendelea yamekuwa  yakiongozwa na viongozi wenye umri mkubwa.

Kamati ya bunge iko inajadiliana muswada ambao unatoa kikomo cha miaka 75 tu kuwa mgombea wa urais nchini humo. 

Wakati wa kutetea hoja yake,Museveni alitoa mfano wa nchi ya Tunisia na kumzungumzia kiongozi wa taifa hilo Beji Caid Essebsi.

Mnamo mwaka 1986 wakati Museveni akiingia madarakani alisikika akisema kuwa tatizo la Afrika na hasa Uganda sio wananchi bali ni viongozi wanaon'gan'gania madarakani.

 Habari Zinazohusiana