Ghasia na fujo vyazuka katika mji mkuu wa Zambia

Ghasia na tafrani katika mji mkuu wa Lusaka vimepelekea maafisa polisi wanane kujeruhiwa.

Ghasia na fujo vyazuka katika mji mkuu wa Zambia

Ghasia na tafrani katika mji mkuu wa Lusaka vimepelekea maafisa polisi wanane kujeruhiwa.

Mkuu wa polisi,Kakoma Kanganja amewaambia waandishi wa habari kuwa fujo hizo zimeanzia  Kinyama.

Kinyama inaaminika kuwa kati ya sehemu kubwa zenye makazi yasio halali nchini Zambia.

Polisi walienda kufunga moja ya masoko yasiyo halali mahala hapo wakati ghasia hizo zikitokea.

Polisi wamekuwa wakifanya hivyo kama njia ya kupamaba na kusambaa kwa ugonjwa wa kipindupindu.

Hata hivyo baadhi ya wakazi wanailaumu serikali kwa kutotoa huduma ya maji safi,hali iliyopelekea mlipuko wa kipindupindu.

Wakazi hao hawakubaliani na njia serikali inayotumia kupambana na ugonjwa huo.

 Habari Zinazohusiana