NGO:Wanawake 510 wamebakwa DRC mwaka 2017

Jumla ya wanawake 510 walibakwa katika mkoa wa Kasai uliojaa mgongano katikati ya DRC mwaka wa 2017, kulingana na ripoti iliyotolewa Ijumaa na Shirikisho la Mataifa ya Afrika ya Haki za Watoto na Wanafunzi (LIZADEEL).

Mratibu wa mkoa wa LIZADEEL Jean-Malhys Lungala amesema kuwa kesi 405 zilihusisha watoto, na waathirika 500 wa unyanyasaji wa kijinsia waliokuwa wametumwa katika vituo vya afya kwa ajili ya matibabu.

'' 80% ya kesi za unyanyasaji wa kijinsia zilifanywa na Kamuina Nsapu [militamen], '' amesema Lungala 

Bwana Lungala Ameongeza kuwa kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Watoto (UNICEF), wameweza kusaidia waathirika wa unyanyasaji wa kijinsia.

UNICEF iliwapa kits ambazo zinazuia maambukizi ya UKIMWI au magonjwa ya zinaa kati ya waathirika wa vurugu.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, kesi 350 zimepelekwa mahakamani huku thelathini zikiwa zimehukumiwa tayari.

Tagi: wanawake , DRC

Habari Zinazohusiana