Ushirikiano baina ya Uturuki na Afrika

Mzozo wa kisiasa nchini Kenya

Ushirikiano baina ya Uturuki na Afrika

Uchambuzi wa Ibrahim Bachir Abdoulaye

Tunatakiwa kuelewa mfumo na jamii tofauti zinazopatikana nchini Kenya ili kuelewa mzozo wa kisiasa uliyoibuka nchini humo.

Kenya ni taifa ambalo lina raia takribani milioini 50, na kuwa na makabila zaidi  ya 50. Makabila makubwa nchini humo ni makabila manne. Makabila yenyewe ni kabila la kikuyu ambalo ni asilimia 22 ya raia wa Kenya, Luhya asilimia 14, Lou asilimia 13 na kabila la  Kalenji likiwa ni asilimia 12 ya raia wa Kenya.

Hadi katika kipindi cha ukoloni makabila hayo nchini Kenya yalikuwa yakiishi kwa usalama na amani.

Katika kipindi  cha ukoloni makabila hayo yalikuwa yakiishi  kwa makundi yaliogawanywa na Uingereza.

Hali hiyo  inaashiria  na kutufanya tuelewe ushindani mkubwa  kwa kikabila nchini Kenya.

Hali yiyo ya kugawanya makabila katika maeneo tofauti  yamepelekea kuundwa makundi tofauti chini ya malengo ya kisiasa.

Uingereza ilipelekea kuundwa kwa vyama vya kisiasa baada ya uhuru  na kupelekea ushindani wa kisiasa  kati ya makabila tofauti kwa malengo ya  kisiasa baada ya uhuru.

Katika kipindi hicho  vyama vya kisiasa  viliundwa na kuongozwa kikabila. Kwa mfano chama cya KANU kilikuwa chama cha kabila la Luo na  Kikuyu chama cha  KADU na makabila mengine  kama Kalenji, Maasai, Turkana et Samburu.

Kenya ni miongoni mwa mataifa barani Afrika ambayo yalikumbwa na ghasia mbaya katika kipindi cha miaka 15 iliopita  kutokana na sababu za kisiasa.

Kenya ilikuta katika  katika matatizo kutokana na siasa ambayo ilitoa nafasi kikabila.

Katika kila kipindi uchaguzi  unapoawadia  suala zima la kikabila linachukuwa hatamu.

Uchaguzi wa kwanza nchini Kenya ulifanyika Mei mwaka 1963. Raia walishiriki katika uchaguzi kwa lengo la kumchaguwa  kiongozi  atakae ungozi taifa kwa uhuru.

Jomo Kenyatta alichaguliwa kuwa rais wa kwanza wa Kenya katika uchagzui huo uliofanyika mara ya kwanza nchini humo.

Chama kimoja cha KANU kimeongoza Kenya  hadi  Jomo Kenyatta alipofariki mwaka 1978. Katika kipindi cha Jomo Kenyatta  chaguzi  zilifanyika.  Katika kipindi hakuna tatizo kubwa lililotokea kutokana na uchaguzi  kama tunavyoshuhudia leo. Baada ya kifo cha Jomo Kenyatta Daniel Arap Moi alichukua  uongozi .

Daniel Arap Moi alishinda uchguzi mwaka 1979.  Daniel Arap Moi aliongoz Kenya hadi miaka ya 1990.  Kutoka na  haliilioonekana kumlazimisha  ndani na nje  miaka ya 1991  kufuata mfumo.

Kutoka na demokrasia , nchini Kenya  matatizo ya kikabila  yamejitokeza kwa kasi  katika ulimwengu wa siasa nchini humo.

Vyama vya kisiasa  vimejitokeza  kwa kujinasibu ukabila. Mwaka 1992. Uchaguzi ulifanyaika na Moi kuchaguli kuwa rais  kwa ailimia 36,8. Mwaka 1997 vyama vya kisiasa nchini humo vilionezeka na kufikia vyama 27.

Hata hivyo Kenya ilipiga hatua ya kidemokrasia katika uchaguzi mkuu wa nchi hiyo wa mwaka 2002. Chama  Tawala cha KANU ambacho kilimsimamisha Uhuru Kenyatta, mtoto wa muasisi wa taifa hilo Bwana Jomo Kenyata alishindwa uchaguzi huo dhidi ya mgombea wa umoja wa vyama vya upinzani, NARC bwana Mwai Kibaki. Aidha kura ya maoni iliyoandaliwa na Mwai kibaki mnamo Novemba 21 mwaka 2005 kupendekeza mabadiliko ya muhula wa Urais wa nchi hiyo, na kushinda kwa asilimia 58 kulileta mapinduzi mengine makubwa kidemokrasia. Uchaguzi wa 2002 pamoja na kura hii ya maoni, vilichangia kwa kiasi kikubwa kuibadili demokrasia ya nchi hiyo. Pamoja na hayo, hali ya kisiasa iliimarika zaidi. 

 

Lakini kutokua na maendeleo makubwa ya kiuchumi, kuongezeka kwa kiwango cha rushwa nchini  pamoja na wananchi kutokua na furaha ni baadhi ya mambo yaloikumba nchi hiyo. Kutokana na hali hii, vyama Vingi vya siasa vilianza kuungana na kuunda umoja ili kuhakikisha uwepo wao hauathiriwi. Mathalani, chama cha kidemokrasia cha PLD kiliungana na chama cha KANU na kuunda chama cha kidemokrasia cha ODM. Baadaye wakati wa uongozi wa Raila Odinga kilijulikana kwa jina la Harakati za Kidemokrsia ODM na wakati wa utawala wa Kalonzo Musyoka kiliitwa chama cha Harakati na Demokrasia cha Kenya WDM-K na kukigawa chama cha ODM katika pande mbili. 

 

Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2007, ambao uliwakutanisha Mwai Kibaki wa Chama cha Umoja wa kitaifa, PNU na Raila Odinga wa ODM; Kenya ilijikuta ikiingia katika mgogoro wa kisiasa. Wakati chama cha ODM kikiungwa mkono na makabila ya wajaluo, Waluhya na Wakalenjini, chama cha PNU  kiliungwa mkono sana na watu wa kabila la Wakikuyu. 

 

Tume ya taifa ya uchaguzi nchini humo, ilipomtangaza bwana Mwai Kibaki kuwa mshindi kwa kujitwalia asilimia 46 za.kura zote, Raila Odinga alipinga matokeo hayo kwa kudai kuwa uchaguzi you haukua huru na haki na kwamba Mahakama ilipendelea upande mmoja. Nchi iliingia katika machafuko ya kisiasa kutokana na hili. Maelfu ya watu walipoteza maisha kutokana na mapigano baina ya pande hizo mbili hasusan katika miji ya Nairobi, Nyanza na Bonde la ufa.

 

Ugomvi wa kikabila baina ya Wakenya tangu ukoloni sio chanzo pekee cha Machafuko ya kisiasa nchini humo. Mambo kadhaa mengine kama vile kuongezeka kwa idadi ya watu, kuongezeka kwa kiwango cha rushwa na ubadhilifu, utumiaji mbaya wa Silaha kwa.wanajeshi dhidi ya raia, propaganda zifanywazo na vyombo vya habari pamoja na matukio mbalimbali ya kihalifu ni moja ya baadhi ya mambo yanayochangia machafuko hayo. Idadi ya watu Kati ya 1000 na 2000 wanakadiriwa kupoteza maisha kutokana na machafuko ya kisiasa ya mwaka 2007. Na serikali ya Kenya ilipata hasara ya takriban dola bilioni 1.5. Mashirika mengi ya kimataifa yaliingia Kati kutatua mgogoro huu. Lea mfano, mnamo mwaka 2008, Umoja wa Afrika ukiwa chini ya uongozi wa Rais wa Ghana bwana John Kufuor, ulijaribu kuanzisha Majadiliano baina ya pande hizo mbili.

 

Uchaguzi wa kwanza wa urais baada ya mabadiliko mapya ya katiba uliofanyika mwaka 2013 ulishuhudia ushindi wa Uhuru Kenyatta kwa asilimia 50.07. Kiongozi mkuu wa Upinzani bwana Raila Odinga hakukubaliana na matokeo haya na kuvitaka vyama vyote vya upinzani kukata rufaa katika mahakama kuu. Hata hivyo Mahakama ilimpitisha Uhuru Kenyatta kama raisi halali wa nchi hiyo. Maazimio yaliyofikiwa baada ya machafuko ya mwaka 2007 yalisaidia kwa kiasi kikubwa kuzuia kutokea kwa machafuko hayo mwaka 2013. 

 

Kwa Mara nyingine tena, Agosti 8 mwaka 2017, Raila Odinga alibwagwa na Uhuru Kenyatta katika uchaguzi mkuu wa nchi hiyo kwa kupata asilimia 54.27 ya kura zote. Takriban watu 40 walipoteza maisha kufuatia maandamano yaliyofanyika baada tu ya kutangazwa matokeo hayo. Matokeo ya uchaguzi huo yalifutwa na Mahakama kuu ya nchi hiyo baada ya kugundulika kuwa haukua huru na haki. Huu ulikua ni uchaguzi wa kwanza kufutiwa matokeo katika historia ya nchi ya Kenya. Kiongozi wa upinzani bwana Raila Odinga aliamua kususia  Uchaguzi wa marudio uliofanywa Oktoba 26 mwaka 2017. 

Tume ya taifa ya uchaguzi ilimtangaza Uhuru Kenyatta mshindi wa uchaguzi huo kwa alama 98.26. Rais Uhuru Kenyatta aliyechaguliwa kwa awamu ya pili aliapa mnamo mwezi Novemba na kuanza kazi mara moja. Hata hivyo Raila Odinga ambaye alisusia uchaguzi huo aliamua kujiapisha mwenyewe kama Raisi wa watu wa Kenya mnamo tarehe 30 Januari 2018 katika viwanja vya Uhuru Park, Nairobi. Baada ya tukio hili, Raila Odinga anakabiliwa na Madai ya kutengeneza serikali hasi. Lea majibu wa maelezo yaliyotolewa na waziri wa mambo ya ndani wa Kenya, yameeleza kuwa tukio lililofanywa na Odinga ni sawa na kupanga kuipindua serikali. Aidha uchunguzi umeanzishwa kupitia kwa wanasheria.

 

Migogoro hii ya kisiasa inapelekea kuzorota kwa uchumi wa  Nchi hio yenye uchumi imara zaidi Afrika  ya Mashariki. 

Shida ya Ukabila ambayo ilianza tangu enzi za ukoloni, imekua tatizo sugu hasa baada ya kufikia hatua ya kuchagua kiongozi kulingana na kabila lake. Lea mfano upinzani uliopo baina ya Uhuru Kenyatta na Raila Odinga, umetokana na upinzani uliokuwepo baina ya baba zao. Ili kurekebisha migongano hii ya kisiasa, ni lazima kutatua tatizo la Ukabila ambalo limekua wivu nchini Kenya. Nchi haina budi kuandaa mijadala itakayopelekea kuyaleta pamoja makabila yoteHabari Zinazohusiana