Jacob Zuma apewa muda wa masaa 48 kuondoka madarakani Afrika-Kusini

Chama tawala Afrika-Kusini champa muda wa masaa 48 rais Jacob Zuma kuondoka madarakani  au kuondolewa kwa nguvu

Jacob Zuma apewa muda wa masaa 48 kuondoka madarakani Afrika-Kusini

 

 

Rais wa Afrika-Kusini Jacob Zuma  apewa muda wa masaa 48 kuondoka madarakani ua kujiuzulu.

Muda huo wa masaa 48 uliotolewa kwa rais Zuma umetolewa Jumanne  tahadhari  kuwa iwapo atagoma kujiuzulu basi ataondolewa kwa kutumia nguvu.

Taarifa  hizo zilitolewa na kituom cha habari cha SABC cha Afrika-Kusini.

Kamati ya uongozi wa chama cha ANC ilifanya mkutano ambapo kulijadiliwa  suala zima kuhusu rais Jacob Zuma.

Mkutano huo ulichukuwa muda wa masaa manane Jumanne  usiku hadi asubuhi.

Katibu mpya wa chama cha ANC Cyril Ramaphosa akishirikiana na Magashule walijielekeza kwa Zuma kumfahamisha kulichoafikiwa katika mkutano wa chama.

Wanachama wa ANC wameseka kuwa Zuma ajiuzulu ili asije akapelekea chama cha ANC kushindwa katika uchaguzi unaotarajiwa mwaka 2019.

Chama cha ANC kinamuona Jacob Zuma kama kizuizi.Habari Zinazohusiana