Kenya kurusha satellite yake ya kwanza

Kenya inatarajia kurusha satellite yake ya kwanza katika historia ifikapo Mei 11

Kenya kurusha satellite yake ya kwanza

Msaidizi Mkuu wa chuo kikuu cha Nairobi Peter Mbith akizungumza na waandishi wa habari amefahamisha kuwa kwa mara ya kwanza satellite iliyotengenezwa na wahandisi wa chuo hicho  wakishirikiana na shirika la JAXA la Japan itarushwa angani kutokea Japan.

Zoezi hilo la kurushwa kwa satellite hiyo litaoneshwa moja kwa moja  kupitia rundinga ya taifa. 

Hatua hiyo ikifanikiwa basi Kenya itakuwa imeingia katika orodha ya mmataifa ya bara la Afrika yaliyowahi kurusha satellite angani.

Mataifa ya bara la Afrika ambayo yalikwisharusha  sattelite ni  Afrika Kusini,Nigeria,Algeria na Misri.Habari Zinazohusiana