Kura ya maoni nchini Burundi yaidhinisha katika kufanyiwa marekebesho

Kura ya maoni yaidhinisha katiba kufanyiwa marekebesho baada ya tume ya uchaguzi kutangaza ushindi wa « NDIO » nchini Burundi

Kura ya maoni nchini Burundi yaidhinisha katika kufanyiwa marekebesho

Tume ya uchaguzi nchini Burundi iliosimamia kura ya maoni iliowataka raia nchini humu kuchangua kati ya « NDIO »  na « HAPANA » kufanyia marekebesho katiba imetangaza kuwa « NDIO » imepata ushindi wa  kwa asilimia 73,6 ya kura. Taarifa ya ushindi wa « NDIO » imetolewa hapo Jumatatu na kiongozi wa tume ya uchaguzi Pierre Claver Ndayicariye .

Kiongozi wa tume ya uchaguzi amesema kuwa  aslimia 96,24 ya watu waliojiandisha kupiga kura  ilipiga kura hiyo iliofanyika Alkhamis Mei 17.

Hakuna ghasia za aina yeyote zilizoripotiwa katika zoezi la upigaji kura.

Upinzani nchini Burundi unapinga katiba kufanyiwa marekebesho ukidai kuwa  katiba mpya  itampa fursa rais Nkurunziza kusalia madarakani hadi mwaka 2034.

Muhulu wa rais kuongoza nchini Burundi uliokuwa miaka mitano utaongezwa na kuwa miaka 7.Habari Zinazohusiana