Seneta ahukumiwa kifungo cha miaka 14 kwa kosa la ulaji rushwa Nigeria

Seneta ahukumiwa kifungo cha miaka 14 gerezani kwa kosa la ulaji rushwa nchini Nigeria

Seneta ahukumiwa kifungo cha miaka 14 kwa kosa la ulaji rushwa Nigeria

 

Seneta ahukumiwa adhabu ya kifungo cha  miaka 14  baada ya kukutwa na kosa la ulaji rushwa nchini Nigeria

Seneta mmoja  aliefahamika kwa jina la Joshua Dariye amehukumiwa adhabu ya kifungo cha miaka 14 gerezani baada ya kukutwa na kosa la ulaji rushwa nchini Nigeria. Seneta huyo aalikuwa  gavana wa jimbo la Kaskazini nchini Nigeria.

 Hamakama imetoa hukumu hiyo  baada ya kumkuta Joshua na kosa la kutumia kiwango cha dola milioni 3,3 kati ya mwaka 1999 na mwaka 2007 alipokuwa gavana wa eneo hilo.

Hukumu hiyo imetolewa bila ya kutoa fursa kwa mshatakiwa kukata rufaa.


Tagi: rushwa , Nigeria

Habari Zinazohusiana