Ethiopia na Eritrea zakubaliana kufungua ubalozi

Ethiopia na Eritrea zimekubaliana kufungua upya balozi katika miji yake mikuu.

Ethiopia na Eritrea zakubaliana kufungua ubalozi

Ethiopia na Eritrea zimekubaliana kufungua upya balozi katika miji yake mikuu.

Baada ya  uhasama wa muda mrefu nchi hizo mbili zimeamua kuweka tofauti  zao pembeni na kudumisha uhusiano baina yake.

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed ambae yupo katika ziara ya siku tatu nchini Eritrea ametangaza kuhusu makuabaliano ya kufungua balozi hizo.

Nchi hizo mbili vilevile zimefungua njia za mawasiliano ambazo zilikuwa zimefungwa kwa zaidi ya miaka 20.

Eritrea ilijitenga  na Ethiopia 1993.Habari Zinazohusiana