Idadi ya watu waliofariki baada ya kivuko MV Nyerere kuzama nchini Tanzania yazidi kuongezeka

Idadi ya watu waliofariki katika jali ya kivuko katika Ziwa Victoria nchini Tanzania yazidi kuongezeka na kufikia watu 207

Idadi ya watu waliofariki baada ya kivuko MV Nyerere kuzama nchini Tanzania  yazidi kuongezeka

Watu 207 wameripotiwa kufariki baada ya  kivuko MV Nyerere kuzama katika Ziwa Victoria nchini Tanzania.

Rais wa Tanzania John Magufuli ametangaza siku nne za maombolezo  kuwakumbuka waliopoteza maisha katika ajali hiyo.

Kulingana na taarifa zilizotolewa na ajili hiyo imetokea kutokana na uzito mkubwa uliosababishwa na abiria wengi kuliko  kiwangokilichowekwa .

Kwa upande wake waziri wa uchukuzi   wa Tanzania Isaack Kamwelwe amesema kuwa juhudi za kuokoa miili ya watu waliozama zinaendelea.

Kamishna wa jiji la Mwanza John Mongella amesema kuwa mtu  mmoja ameokolewa akiwa hai.

MV Nyerere imezama Alkhamis majira ya alasiri.

 Habari Zinazohusiana