Mohammed Dewji atekwa na watu wasiojulikana nchini Tanzania

Kijana tajiri miongoni mwa matajiri barani Afrika Mohammad Dewji atekwa  nchini Tanzania

Mohammed Dewji atekwa na watu wasiojulikana nchini Tanzania


Mohammad Dewji, bilionea kijana  atekwa na watu wasiojulikana mjini Dar Es Salaam nchini Tanzania.

Mohammad Dewji atekwa  na watu waliojuwa na silaha ambao pia walikuwa wamefunika nyuso zao.

Bilionea huyo mwenye umri wa miaka 43 ametekwa  mapema asubuhi ya Alkhamis mjini Dar Es Salaam nchini Tanzania.

Mfanyabiashara huyo ambae anatambulika kama Mo Dewji nchini Tanzania ametekwa majira ya asubuhi alipokuwa akijielekeza mazoezini .

Taarifa hiyo imetolewa na vyombo vya usalama nchini Tanzania.

Watu watatu wamekwishakamatwa kufutia tukio hilo.

Waziri wa mazingira January Makamba amethibitisha kuwa Dewji alizungumza na wazazi wake  na familia yake kuwa kweli ametekwa.

Dewji ni miongoni mwa vijana matajiri barani Afrika ambao wameinua kiuchumi  mataifa yao kwa kuwekeza katika biashara. 

Kulingana na taarifa ambazo zimetolewa, raia wawili wa kigeni wanashukiwa kuhusika na kumteka bilionea huyo.

Jeshi la Polisi linaendelea na  msako. Habari Zinazohusiana