Waziri wa ulinzi wa Uturuki akiwa nchini Libya

Waziri wa ulinzi wa Uturuki amefanya mkutano na maafisa wa Libya katika mji mkuu wa Tripoli.

Waziri wa ulinzi wa Uturuki akiwa nchini Libya

Waziri wa ulinzi wa Uturuki amefanya mkutano na maafisa wa Libya katika mji mkuu wa Tripoli.

Kulingana na wizara ya ulinzi,Hulusi Akar amekutana na maafisa kama Fayez al-Sarraj ambae ni kiongozi wa baraza la Urais na kujadili masuala mbalimbali.

Akar vilevile amekutana na waziri wa mambo ya ndani wa Libya Fatih Ali Bashagha na kiongozi wa halmashauri kuu ya nchi Khalid al Mishri.

Katika mkutano huo,ushirikiano kati ya mataifa hayo mawili hasa katika sekta ya ulinzi ilikuwa ni kati ya mada muhimu zilizowekwa mezani.

Hivi sasa, viti viwili vya upinzani vyenye nguvu vinawania utawala nchini Libya: serikali ya umoja wa kitaifa  iliyoko Tripoli, na serikali ya "muda mfupi" inayoungwa mkono na chombo cha sheria kilichopo mashariki mwa Tobruk.

Serikali ya Tobruk ilianzishwa rasmi mwaka 2016 ikiongozwa na Al Sarraj.

 Habari Zinazohusiana