Baada ya miaka 41,"Ethiopian Airlines" yaanza safari kuelekea Mogadishu

Shirika la ndege la Ethiopia limetangaza kwamba linaendelea tena na safari zake kuelekea Mogadishu, mji mkuu wa Somalia, baada ya kuwa safari hizo zilisimamishwa kwa muda wa miaka 41.

Meneja Mkuu wa Ndege hizo,Tewolde Gebremariam amesema kuwa safari za ndege kati ya Addis Ababa, mji mkuu wa Ethiopia, na Mogadishu zimeanza rasmi.

Gebremariam amesema ndege hizi zitachangia katika kuendeleza mahusiano kati ya nchi hizo mbili.

Abiy Ahmed, aliyechaguliwa kama waziri mkuu nchini Ethiopia, alitembelea Rais wa Somalia Mohammed Abdullah Fermacu mwezi Juni ili kuboresha mahusiano na Somalia.

Mnamo mwaka 1977 jeshi la Somalia lilimiliki eneo la Ogaden, ambako makabila ya Somalia yaliishi, na baadae jeshi la Ethiopia lilifanya shambulizi  na kulichukua tena eneohilo.

Kufuatia mgogoro huo, mahusiano ya kidiplomasia yalikatwa kati ya nchi mbili na safari za ndege zilifutwa.Habari Zinazohusiana