Shambulizi la bomu Somalia

Watu takriban 23 wameripotiwa kupoteza maisha na wengine wengi kujeruhiwa baada ya magari matatu kulipuka katika mji mkuu wa Somalia.

Shambulizi la bomu  Somalia

Watu takriban 23 wameripotiwa kupoteza maisha na wengine wengi kujeruhiwa baada ya magari matatu kulipuka katika mji mkuu wa Somalia.

Afisa wa polisi mjini Mogadishu Abdullahi Mohamed amekiambia kituo cha habari cha Anadolu kuwa mabomu hayo yalikuwa yameilenga hoteli ya Sahafi na baadaye.

Kwa mujibu wa habari,baada ya milipuko hiyo umwagaji wa risasi ulifuatia.

Hoteli hiyo ipo karibu na makao makuu ya  idara ya uchunguzi wa wahalifu nchini humo.

Kati ya waliopoteza maisha baadhi walikuwa ni maafisa polisi na wengine raia wa kawaida.

Majeruhi wamekimbizwa hospitalini.

 Habari Zinazohusiana