Mashambulizi ya Boko Haramu yapelekea hasara kubwa nchini Nigeria

Nemi Osinbajo,makamu wa rais wa Nigeria amesema kuwa nchi yake imepata hasara ya dola bilioni 9 katika sekta ya miundombinu kutokana na mashambulizi ambayo yamekuwa yakifanywa na kundi la kigaidi la Boko Haramu nchini humo.

Osinbajo katika hotuba aliyotoa mjini Abuja ameongeza kwa kusema kuwa zaidi ya watu milioni mbili wamelazimika kuyahama makazi yao kutokana na mashambulizi hayo.

"Kundi la Boko Haram limesababisha vifo vya watu 20,000 ndani ya miaka 10 iliyopita kutokana na mashambulizi ya hapa na pale.Hasara iliyoletwa na mashambulizi ya magaidi hao nchini Nigeria ni kubwa.Zaidi ya majumba 400,000,mahospitali na ofisi za umma vimeangamizwa",alisema Osinbajo.

Hata hivyo ripoti ya jeshi la  nchi hiyo imeonyesha kuwa mashambulizi ya magaidi hao yamepungua kwa asilimia 83 ikilinganishwa na ilivyokuwa mwaka 2014..

 Habari Zinazohusiana