40 wapoteza maisha kwenye maandamano nchini Sudan

Mashirika ya misaada ya kimataifa yaripoti kwamba watu 40 wamepoteza maisha kwenye maandamano nchini Sudan

40 wapoteza maisha kwenye maandamano nchini Sudan

Maandamano dhidi ya utawala yameendelea nchini Sudan. Siku ya jana  mikoa mingi kuanzia na  Khartoum kaskazini yalifanyika maandamano yenye lengo la kuupinga utawala uliopo madarakani.

Kwa mujibu wa shududa, vyama vya upinzani, vyama vya kitaaluma vya madaktari, waalimu na wahandisi vilitisha maandamano katika miji ya kaskazini mwa Khartoum, El Fao,El Fashir pamoja na Amri. Maandamano hayo waliyaitisha katika wiki maalum waliyoiita kama " wiki ya mageuzi katika miji, vijiji na wilaya"
Katika maandamano hayo yaliyohudhuriwa na maelfu ya watu ulinzi mkali uliimarishwa.

Katika kukabiliana na waandamanaji polisi walitumia mabomu ya machozi. Watu wengi wanashikiliwa na polisi kutokana na maandamano hayo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na vyama vya kitaaluma maandamano yao yalifanyika katika miji Khartoum kaskazini, El Fao, El Fashir na Amri.

Maandamano nchini Sudan yalianza mnamo Desemba 19, yalianzishwa kupinga kupanda kwa bei ya mkate katika miji ya pwani ya mto Nile, Atbera na Port Sudan, lakini baadae yalienea nchi nzima na lengo sasa likiwa ni kuipinga serikali.

Mamlaka nchini Sudan zinasema katika maandamano hayo watu 24 wamepoteza maisha, Huku mashirika ya misaada ya kimataifa yakisema waliopoteza maisha ni 40.Habari Zinazohusiana