Mtazamo wa Uturuki kwa Mashariki ya kati

Madhara ya mashambulizi ya angani ya vikosi vya Urusi na utawala wa Assad

Mtazamo wa Uturuki kwa Mashariki ya kati

Takriban miezi minane iliyopita daktari mmoja kutoka Syria alitamka haya “Aleppo sasa inaishi katika enzi za uhaba na uwepo wa majeneza pekee!”

Tangu Aprili Mwaka 2016 wakaazi wa Aleppo wamekuwa wakiishi na taswira za kutisha za vifo na mabomu ya kila siku .Shirika la kimataifa la huduma ya kwanza kwa mtazamo huo lilichapisha ripoti na kufahamisha kuhusu taarifa muhimu.

Katika ripoti hiyo ilielezea kuwa serikali ya Assad  wakishirikiana na vikosi vya Urusi walikuwa wanalenga vituo vyote vya afya na hospitali zote zilizokuwa katika mji huo wa Aleppo.Kwa mujibu wa ripoti ya shirika hilo ni kuwa ilikuwa mojawapo ya mipango ya utawala wa Assad na Urusi kushambulia hospitali hizo kabla na hata baada ya ilani ya kusitishwa kwa mapigano. Urus na Assad walishambulia kila upande wa Aleppo na kuhakikisha kuwa hamna hata umeme wala maji ya kunywa katika hospitali hizo na hivyo basi wakaazi wakalazimika kuhamia maeneo mengine.

 

Siku kadhaa zilizopita, rais wa Urusi Vladimir Putin alitangaza mpango wa kutaka kuondoa wanajeshi wake nchini Syria. Putin alibainisha kukamilisha harakati zake za operesheni kwa mafanikio nchini Syria na kwamba ataweza kuondoa wanajeshi wake. Wakati huo huo, Urusi pia ilitangaza kuendeleza harakati zake kwenye kambi za vikosi vyake vya majini na angani nchini humo.

 

Putin amedhihirisha kukamilisha lengo la Urusi. Hivyo basi, baada ya hatua hiyo sasa Urusi inapaswa kufauata njia kidiplomasia. Je, kwa mtazamo huu unadhani ni sababu gani iliyofanya Urusi kuona njia hii wanayoifuata sasa kuwa tofauti na njia iliyofuatwa miezi sita iliyopita?

 

Tangu Urusi kuanza kuendesha operesheni zake nchini Syria mwezi Septemba mwaka 2015, utawala wa Assad umeonekana kupata fursa ya kuimarika tena. Upinzani wa Syria pamoja na vikosi vyake vimeweza kupata pigo kubwa kutokana na mashambulizi ya angani yaliyotekelezwa na vikosi vya Urusi. Kutokana na harakati hizo dhidi ya upinzani, utawala wa Assad uliweza kupata nguvu upya na kufanikiwa kudhibiti takriban maeneo 400 ya makaazi yaliyokuwa mikononi mwa upinzani. Kulingana na maelezo ya Kremlin, utawala wa Assad uliokuwa umepoteza nguvu dhidi ya upinzani nchini Syria mwaka jana umeweza kusimama tena imara kwa sasa. Hata hivi karibuni eneo zima la Aleppo linaonekana kuwa tayari kudhibitiwa na vikosi vya utawala wa Assad nchini humo.

 

Ni wazi kwamba Urusi iliingilia kati mapambano kati ya vikosi vya utawala wa Assad na upinzani wa Syria pasi na kutaka kujihusisha na vita hivyo kwa muda mrefu. Hawakutaka kujipata katika hali kama ya Afghanistan iliyoendelea kwa miaka mingi. Ni wazi kwamba Urusi ingeweza kusaidia utawala wa Assad hadi mwishoni mwa mwaka wa 2016 kutokana na hali ya uchumi iliyokuwepo. Kwa kifupi Urusi imeweza kukomboa utawala wa Assad kwa kuupa nguvu zaidi dhidi ya upinzani.

Tukitazama matukio yote kwa kwa makini zaidi tunaona kwamba Marekani imekuwa ikipinga harakati za Urusi za mashambulizi na operesheni nchini Syria ingawaje Marekani pia haikupinga hatua ya Uusi kuingia Syria na kuunga mkono utawala wa Assad hapo mwanzoni. Hata Marekani iliunga mkono utawala wa Assad kusaidiwa kwenye mapambano dhidi ya DAESH ingawaje haikutaka kuchukuwa hatua hiyo.

 

 

 

Ndani ya miaka 5 ya mashambulizi nchini Syria mamia ya madaktari katika nchi hiyo wamepoteza maisha .Kwa mujibu ya ripoti iliyotolewa ni kuwa takriban madaktari 701 nchini Syria wamepoteza maisha yao katika mashambulizi.Kwa ujumla mashambulizi 382 ya angani yametekelezwa na katika mashambulizi hayo takriban hospitali 269 zimeharibiwa .Ndani ya mwezi Desemba pekee jumla ya mashambulizi 54 yametekelezwa.

Juma lililopita utawala wa Assad ulitangaza kuchukua udhibiti wa kanda ya mashariki ya mji wa Aleppo.Hii ina maana kuwa jumuiya ya kimataifa ina jukumu kubwa zaidi kuto sauti kuhusu hali hii.Hata hivyo la kusikitisha ni kuwa imekuwa wazi kuwa jumuiya magharibi imekuwa haijali masuala kama haya jambo ambalo hata halihitaji tena kzngumziwa katika bunge tena .

Kuhusu suala hili waziri wa fedha wa zamani wa uingereza George Osborne alisema kuwa

“Ikiwa tunaamini kuwa hatujasababisha yanayoendelea Syria basi tunajidanganya ,kwani janga la Aleppo ni janga lililoanzishwa na Marekani,Uingereza na magharibi kwa ujumla .”

 Habari Zinazohusiana