Uchambuzi wa Matukio

Uchambuzi wa Matukio

Uchambuzi wa Matukio

Miezi miwili iliyopita onyo lilitolewa kuwa ugaidi sasa si tishio kwa Uturuki na Mashariki ya Kati pekee bali kwa dunia nzima kwa ujumla .

Leo hii tunakumbwa na ugaidi wa hali ya juu katika historia ya dunia.Makundi ya kigaidi katikakarne ya sasa na mpango na uongozi wa kitaaluma na ustadi wa hali ya juu.Hapa tunaongelwea kuhusu makundi ya kigaidi yaliyoundwa kwa misingi ya kuweza kuingia katika taaluma na taasisi nyingi za mataifa kote duniani.

Makundi haya ya kigaidi yameundwa kwa namna ya kuwa yanapatikana katika jamii zote z akidini iwe Uislamu,Ukristo na hata Budhi.

La kusikitisha ni kuwa kundi hili la kigaidi hutumia imani nzuri na mfumo wa dini zilizopo katika dini.Kundi hili la kigaidi lianendelea kuingia katika mshirika tajiri zaidi ya Umoja wa Ulaya hadi katika maeneo y mbali barani Afrika .

Kundi hili ni kundi la kigaidi la FETÖ.Kiongozi wa kundi la FETÖ ni Fetullah Gülen anayeishi katika Kasri moja katika mojawapo ya makasri ya Marekani.

Viongozi wengine katika kundi hili pia wanapatikana katika majumba ya kifahari barani Ulaya kama Uingereza,Canada,Scandanavian na kadhalika .

 

Viongozi wa kundi la FETÖ wametorokea na kujificha katika mataifa mengi ya magharibi miongoni mwao EU mataifa yanayojivunia kuwa na serikali za kidemokrasia.

Viongozi hawa kutoka mataifa haya wanapanga misururu ya mashambulizi ya kigaidi na kupelekea maelfu kufariki huku huzuni na mateso kuendelea nchini Uturuki.

Kwa mfano nchi jirani ya Uturuki nchi ya Ugiriki bado haijawarudisha magaidi waliotorokea nchini hum ona waliosababisha vifo vya raia wengi wa Uturuki na kutishia hata maisha ya rais Recep Tayyıp Erdoğan .

Magaidi hawa baadaye hutembea katika mazulia mekundu ya watu muhimu katika nchi hizo na baadaye kupewa ulinzi na vibali vya pasipoti.

Magaidi hawa ni magaidi walio na uwezo wakubisha hodi katika milango ya bunge la Ulaya na kukaribishwa bila wasi wasi wowote .

Viongozi nchini Uturuki wakiongozwa na rais wa Uturuki Recep Tayyıp Erdoğan mara kwa mara hutoa wito kwa mataifa ya magharibi na kusisitiza kuwa chamgamoto ya ugaidi si Uturuki pekee bal ini tatizo kwa dunia nzima kwa ujumla .

Rais Erdoğan kila mara ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuungana na kupiga vita ugaidi wa aina yoyote .

A kushangaza kuwa Umoja wa Ulaya hupendekeza kuzingatia ubinadamu na sera zao za Magharibi lakin imara kwa mara wanapuuza wito wa Uturuki.Katika hotuba zao za kidiplomasia wameonekana wazi kutumia maneno ya kejeli dhidi ya rais Erdoğan.Hata hivyo hadi kufikia sasa magaidi wa kundi hili wameonyesha kuwa hawatochelewa kutekeleza mashambulizi ya kinyama hata Ulaya kutoka Ugiriki hadi Ubelgiji,na kuuwa wanawake kwa watoto ,wakubwa kwa wazee.

Baada ya Urusi na Uturuki kugundua kuwa mvutano ulioletwa na kuangushwa kwa ndege ya Urusi na jeshi la Uturuki ilikua mbinu ya kugonganisha ,Moscow na Ankara waliamua kukaa chini ten ana kuboresha mahusiano .

Hata hivyo hatua hiyo ya Urusi na Uturuki imeonekana kutoridhisha kundi la FETO na kwa mara nyingine wametumia mbinu nyingine ya uchochezi na kupanga mauaji ya balozi wa Urusi jijini Ankara Andrei Karlov.

Usiku wa shambulizi katika hafla ya ufunguzi wa maonyesho ya picha jijini Ankara,huku mauaji ya balozi Andrei Karlov yakitekelezwa jijini Berlin nchini Ujerumani kulitekelezwa shambulizi lingine la kigaidi ambapo watu zaidi ya kumi walipoteza maisha na wengine kadhaa kujeruhiwa .

Wakati huo huo nchini Jordan kadhaa walifariki katika shammbulizi,huku nchini Uswisi kukatokea shambulizi katika msikiti mmoja jijini Zurich na kadhaa walijeruhiwa .

Wanaowapokea magaidi wanahusishwa na mauaji ya maelfu ya watu wasio na hatia ikiwa ni pamoja na balozi Andrei Karlov.

 Habari Zinazohusiana