"Juhudi za Uturuki zimepelekea kuondoa raia 44 000 Aleppo"

Juhudi za kidiplomasia za Uturuki zimepelekea kuokoa na kuondoa raia waliokuwa wamezuilika katika mji wa Aleppo

"Juhudi za Uturuki zimepelekea kuondoa raia 44 000 Aleppo"

Juhudi za kidiplomasia za Uturuki zimepelekea kuokoa na kuondoa raia waliokuwa wamezuilika katika mji wa Aleppo.

Raia takriban 44 000 waliweza kuondolewa katika mji wa Aleppo kutokanana juhudi za kidiplomasia za serikali ya Uturuki.

Msemaji wa ikulu ya rais mjini Ankara İbrahim Kalın amefahamisha ya kwamba raia zaidi 44 000 wameweza kuondolewa mjini Aleppo  na kuhamishiwa katika mji wa Idlib kutokana na juhudi za kidiplomasia za Uturuki.

Raia hao waliondolewa katika mji huo kutokana na hali mbaya ya usalama katika eneo hilo kwa muda mrefu.

Msemaji wa ikulu mjini Ankara İbrahim Kalın alifanya mkutano na waandishi wa habari alifahamisha kuwa hatua zote zilichukuliwa ili  kukidhi mahitaji muhimu ya raia hao waliohamishwa kutoka mjini Aleppo.

Alifahamisha kuwa hatua ya mwisho ya operesheni ya Fırat katika mji wa al Bab ni kwa niaba ya kupambana na kundi la wanamgambo wa kundi la kigaidi la Daesh.

İbrahim Kalın alizidi kufahamisha kuwa uhaba wa mashambulizi ya anga katika operesheni ya Azzez-Jarabluz hutupiwa lawama kila wakati ambapo kunaendeshwa mashambulizi dhidi ya Daesh.

Mashambulizi na mapambano kwa sasa yameonekana kukita mizizi al Bab juma hili.

 Habari Zinazohusiana