« Mwaka wa majanga na umwagaji damu ulimwenguni »

Uchambuzi wa matukio na msemaji wa ikulu ya rais mjini Ankara

« Mwaka wa majanga na umwagaji damu ulimwenguni »

Uchambuzi wa matukio na msemaji wa ikulu ya rais mjini Ankara

Msemaji wa ikulu ya rais mjini Ankara Ibrahim Kalın katika uchambuzi wa matukio amefahamisha kuwa mwaka 2016 ulikuwa ni mwaka wa majanga na umwagaji damu ulimwenguni.

Mwaka 2016 ulikuwa mwaka wa majonzi na maafa kote ulimwenguni. Mwaka 2016 ulikumbwa na na mashambulizi ya kigaidi huku na kule katika maeneo tofauti ulimwenguni.

Mwaka 2016 ulikumbwa na matendo ya kigaidi yaliosababisha maafa, wimbi la wakaimbizi na wahamiaji haramu, vita baridi bain aya mataifa makubwa, utafauti katika hali ya kiuchumi na kusababisha  mvutano mkubwa  katika nyanja za kimataifa.

Vile vile mwaka 2016 ulikuwa mwaka ambao maisha ya watu wasiokuwa na hatia yaliwekwa katika hatari.

Watu wengi walizuiliwa kufikia malengo yao kutokana na dhulma ilikuwa imetanda.

Ibrahim Kalın amefahamisha ya kwamba iwapo tutataka mwaka 2017 uwe ni mwaka wa matumaini ya kudumu  na kuwa tofauti na mwaka 2016 basi ni wajibu kwetu kulinda ubinadamu.

Tunatakiwa kutoa hadhi hiyo ya ubinadamu ili kuweza kufikia kunako malengo licha ya kujali imani tofauti, utamaduni bali tunatakiwa kutazama taifa letu kwa mtazamo mmoja.

Mfumo wa kimataifa katika kipindi hiki unaonekana kuwa katika hali isioridhisha.

Mfumo wa Umoja wa Mataifa umeoneka kudumaa na kutokuwajibika kama ipasavyo.

Inaoneka kwamba Umoja wa Matifa uahitaji kufanyiwa marekebisho ila suala hilo limeoneka pia kufumbiwa mamcho na wala hakuna harakati za kuzungumzia suala hilo. Baadhi ya mashirika ya Umoja wa Mataifa yanajitahidi kuwajibika ipasavyo  licha ya kuonekana kuwa uongozi katika Umoja huo kupuuziabaadhi ya mahitaji katika maeneo ambayo yanahitaji kuungwa mkono katika kujikwamua.

Marekani na Ulaya hawakuweza kuzuia mapambano na uhalifu  katika mzozo wa Syria.

Kunako mzozo wa Iraq, mzozo wa Ukraina, ugaidi katika nyanja ya kimataifa, udukuzi, kuibuka kwa mara nyingine kwa ubaguzi, chuki dhidi ya uislam na waislamu pia miongoni mwa masuala yatoa masuali.

Ulaya kwas asa imeonekana kuwa na ukosefu wa uongozi na malengo.  Imeonekana kwamba Ulaya katika ujumla wake haiwezi kuchukua hatua yeyote  bila ya kushirikisha serikali ya Washington.

Kutokana na kwamba hali ya kisiasa inayojitokeza katika uongozi wa Obama, hali ya usalama katika nyanja ya kimataifa imezidi kudidimia.

Tunasubira kuona vip utawala wa Trump utakavyo ongoza na kutaraji hali ambayo itaridhisha pande zote katika ushirikiano.

Imeoneka kukosekana kwa utulivu katika kipindi fulani.

Ukosefu wa malengo, mtazamo na uongozi umeonekana kutokana na Umoja wa Ulaya kushindwa kuelekeza kunako malengo na harakati ya Uturuki kujiunga na umoja huo.

Kumeoneka pia kushindwa kutatua mzozo katika mkataba na utekelezwaji wake kuhusu suala la wahaimiaji na wakimbizi bain aya Umoja wa Ulaya na Uturuki.

Umoja wa Ulaya umefumbia macho vitisho vya kundi la kigaidi la PKK, kundi la kigaidi la Daesh na kundi la wahini la FETÖ huku baadae kutaka kutoa funzo la demokrasia kwa Uturuki.

Wawakilishi wa makundi hayo na wafuasi wake bado wanasafiri wakiwa huru katika miji mikuu ya Ulaya.

Wakimbizi na wahamiaji katika baddhi ya miji ya Ulaya wananyanyaswa licha ya kujinasibu kuheshimu haki za binadamu.

Mwaka 2017 nchi nyingi za Ulaya zitakuwa katiak uchaguzi mkuu ambapo pia kunazidi kuonekana kuibuka kwa makundi ya mrengo wa kulia yenye misimamo mikali ya kibaguzi dhidi ya uislamu na wahamiaji.

Hali hiyo ya kisiasa Ulaya  kuhusu mabadiliko itadhihirika barani humo.

Uturuki imemmaliza mwaka 2016 ikiwa na kumbukumbu mbaya za jjaribio la mapinduzi ya Julai 15 yalioandaliwa na wahaini wa kundi la FETÖ.

Vile vile mashambulizi kadhaa ya uhalifu yaliotekelezwa na makundi ya kigaidi kama Daesh na PKK.

Washirika wa Magharibi wa Uturuki katika shirika la NATO walishindwa kuinga mkono Uturuki katika kuapambana vitisho vya kigaidi.

Ni wazi kuwa wamesahau ya kwamba usalama wa Uturuki ni uti wa mgongo pia wa usalama wa Magharibi.Habari Zinazohusiana