Uchambuzi wa matukio

Sera za Marekani zimeendeleza uharibifu badala ya kujenga Mashariki ya Kati

Uchambuzi wa matukio

Mkataba wa Yalta uliotiwa saini baada ya vita vikuu vya pili vya dunia ulififia na hata kufilisika baada ya muda wa nusu karne .Sasa hivi unaendelea kuathiri mabilioni ya watu licha ya kuwa inatumika kando kando.Mkataba wa Yalta uliundwa mnamo mwaka 1945 na baadaye mwaka 1991 kiongozi wa kisovieti Mikhail Gorbachev pamoja na sera za Perestroika zikatupilia mbali mkataba huo.Hata hivyo hatua hiyo ilikuwa ya ghafla na mataifa 5 makuu wakarti huo yalipatikana hali ya kuwa hayakutaraji wala kujiandaa kwa mabadiliko hayo.

 

Hii ilipelekea kuwa na pengo ambalo liliathiri kiasi kikubwa uchumi na sekta ya viwanda ya mataifa ya nguvu zaidi duniani.Hivyo basi mpango mpya ikabidi kuundwa na mpango huo mpya ulikuwa Marekani.Marekani ilikuwa na serikali kwa muda wa miaka 200.Hii inamaanisha kuwa serikali yake bado ilikuwa haipo imara zaidi,uundaji wa serikali iliyoimarika kunahitajika takriban awamu 8 ambazo ni sawa na miaka isiyopungua 400.

 

Serikali ya Marekani haina muundo wowote wa kitamaduni wala hata kuwa na muundo wa elimu ya jamii,ni serikali inayoongozwa na  wafanyabiashara ,familia tajiri zilizohamia nchini hum ona wakulim wanaomiliki maelfu ya mahekari ya ardhi.

 

Fukuyama na Hutington zilitumika kuhalalish sera mpya duniani.Mbinu hizo zilitumika kuonekana sawa mbele ya macho ya jamii na dunia nzima kwa ujumla.Hatimaye mbinu hiyo mpya pole pole iligeuzwa na kuingizwa katika ulimwengu wa kisiasa na kutumika kwanza kabisa kipindi cha Uongozi wa Bush.Kipindi hicho Marekani ilivamia Iraq na kutangazwa kuwa ilikuwa ‘Vita vitakatifu’ yani kwa kifupi ilikuwa mbinu ya mkataba wa Yalta wa mwaka 1945.

 

Lakini itambulike ya kwamba sera za Ulaya zilianzishwa hata wakati wa Magna Carta na George Herbert Walker Bush kipindi ambacho Iraq ilianza kuvamiwa mnamo mwa 1991.Wakati huo sauti kutoka vitengo tofauti zilisikika kwa mfano kutoka waandishi,vyuo vikuu na hata wanaharakati ambao walipinga sera hii mpya ya magharibi.Kwa mfano mwanaFalsafa kutoka Uhispania Santiago Alba Rico alipinga vikali sera hii mpya ya dunia.Hivi karibuni Rico amefahamisha kuwa mbinu mpya inayotumiwa duniani ni ya ‘Uwizi wa kimabavu na wanywaji damu  

Kusema ukweli lilikuwa jambo la kushngaza kuona kuwa bado mataifa ya kikomunisti kuwa na mali asili za nishati na njia za nguvu za biashara hata baada ya kumalizwa kwake na pia bado kuwa na migigiro ya ndani yaliyopelekea kuwa na vita ,mapigano,ghasia na mizozo ya kila aina .Kwa upande mwengine mataifa kama Algeria na Afganistan matukio ya kigaidi yakaanza kusikika na kukithiri kila siku.Mnamo Desemba 6 1993,katika gazeti la Independent katika ukurasa wa kwanza na wa kumi wazua maswali mengi .

Katika ukurasa wa kwanza Usama bin Laden na wafuasi wake wanatambulishwa kuwa waleta amani,Kwa habari pia Bin Laden pia anatajwa kuwa mtakatifu akiwa na magaidi .

Miaka ya 1980 Saddam Hussein alitajwa kuwa ‘Mpiganaji shujaa’ alipokuwa mpinzani mkuu wa utawala wa Iran.Ghafla baada ya muda watu hawa waliotajwa na magharibi kuwa ‘Watakatifu’ wanaanza kutangazwa kuwa magaidi.Muda mfupi baadaye Bush anageuza  maeneo haya kuwa mpira wa moto.

 

.

Miaka hiyo pia kundi la kigaidi la FIS laibuka Algeria huku jina la Uislamu pia likitumika kuwakilish kundi hilo .Makampuni ya mafuta ya Marekani yanasimamisha mikataba yao na Alger ia na huku wakikata mikataba hiyo wanatumia mbinu katili kwa silaha kama visu,wafuasi wa FIS waliuawa kwa mauaji ya kimbari kipindi hicho.Kwa bahati mbaya marais na viongozi wote wa Marekani  ni mabepari na viongozi waliotayari kunyakua vitu kimabavu .

 

 Habari Zinazohusiana