Uchambuzi wa matukio

Uchambuzi wa matukio

Uchambuzi wa matukio

Januari 20 ni tarehe muhimu mwaka huu hasa kwa Syria ,Iraq na kanda ya Mashariki ya Kati ,na pia ni siku ambayo Donald Trump ataapishwa kuwa rais rasmi wa Marekani.Ni wazi kuwa sasa kutakuwa na matarajio mapya .Viongozi wapya wanatarajiwa kufanya mabadiliko na kutatua matatizo makuu ya dunia.

Bila shaka Uturuki na Urusi wakishiriana na Iran wamepiga hatua kuu kufanya mabadiliko kuanzia mwaka huu.Nchi hizi zimeweza kuafikiana na wapinzani pamoja na Utawala wa Syria kusitisha mapigano ya miaka mingi nchini humo.

Mnamo Desemba 23 waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergey Ryabkov alifahamisha kuwa Urusi,Uturuki na Iran haina ajenda ya siri kwa Syria na kuwa magharibi sharti ikubali makubaliano ya Syria .

Hivi karibuni Putin alikubali na kutambua kuwa Marekani ni nchi yenye nguvu zaidi duniani.Vladimir Putin alifahamisha haya katika kongamano la kiuchumi  mjini Petersburg.Putin aliendelea kufahamisha kuwa hata Marekani na Urusi wanafa kuungana katika kufanya makubaliano lakini Obama na timu yake imekuwa ikichukua muda mwingi kuitikia wito wa Urusi .Marekani ,Urusi na Iran wanaweza kufanya ushirikiano na hata kutatua tatizo la Syria .Hata hivyo Uturuki haifai kuonekana kama sababu ya kudhooofisha uhusiano baina ya Urusi na Marekani.

Hii ilionekana katika makala yaliyochapishwa katika gazeti la Washington Post,’Jinsi Obama amelazimu Uturuki kuangukia mikononi mwa Urusi.’

Mauaji ya balozi wa Urusi jijini Ankara yamebainishwa kuwa ilikuwa kitendo cha kukosanisha Uturuki na Urusi ,katika tukio kama hilo lililkuwa ni jambo muhimu kufanya ili kuzuia kuingia katika mtego ambao walikuwa wanashuhudia wakati huo.

Kuna matukio muhimu mwaka jana yalitokea ambayo sharti tuyaangalie kwa makini,

Kwa mfano Desemba 16 Marekani na CIA iliomba radhi Uturuki kwa kuishutumu kufanya biashara na kundi haramu la DAESH,lakini Urusi haikuruhusiwa kuomba msamaha kwa Uturuki kwa sababu hiyo hiyo.

Desemba 19:Obama “Uturuki ina jeshi lenye nguvu lakini haijaleta ustawi nchini Syria”

Desemba 19:Ndege ya kivita ya Urusi yaanguka Siberia ikiwa imebeba watu 39 .

Desemba 19:EU yatangaza muda wa kuwekea vikwazo Urusi umeongezwa.

Desemba 19:Urusi yatangaza kuwa mradi wa Uturuki utaendelezwa na kuwasilishwa Duma .

Desemba 19:Balozi wa Moscow jijini Ankara Andrei Karlov  auawa .

Desemba 19:Afisa katika wizara ya mambo ya nje apatikana amefariki jijini Moscow .

Desemba 21 :Mawasiliano baina ya Moscow na Washington yasitishwa .

Desemba 24:Inspekta wa NATO Yves Chandelion auawa kwa risasi alipokuwa anaelekea Ubelgiji.

Desemba 25:Ndege ya kivita ya Urusi aina ya Tupolev Tu-154 iliyokuwa na abiria 93 yaanguka bahari nyeusi .

Desemba 26:Tahadhari ya bomu jijini Moscow,raia waondolewa katika vituo 3 vya treni.

Desemba 26: Haydar Jabar apatikana amefariki katika ubalozi wa Iraq jijini Moscow .

Desemba 23 :Rais Putin katika mkutano kuhusu matukio ya mwaka akiri kuwa muungano wa Uturuki na Urusi umezua matunda hasa katika kutatua matatizo ya Syria.

Desemba  24: Rais Erdoğan atangaza kuwa baada ya Januari 20 uongozi unabadilika Marekani na kufahamisha kuwa watafanya mkutano .Katika mkutano huu tayari Al Baba tumemaliza nas asa imebaki kwenda Munbich ,tutashirikiana na Marekani kusafisha Raqq.

 

Mauaji ya balozi wa Urusi Ankara umeonekana uchochezi ili kusababisha mvutano baina ya Urusi na Uturuki.vilevile imeeleweka kuwa ili kuwa na lengo la pia kuathiri mahusiano baina ya Urusi na Marekani au Trump na Moscow .

Mshambuliaji na waliosaidia kutekeleza shambulizi hilo walikuwa na lengo la kuleta mgogoro mpya uanohusu Uturuki,Urusi na Iran .Nchi hizi tatu hivi sasa zinafanya juhudi kwa pamoja kutatua mgogoro wa Syria .Hapa mpango ulikuwa kuharibu nchi mbili zenye nguvu.Sera ya diplomasia ya Trump itaingia uongozini baada ya Januari 20 na kuna uwezekano mkubwa kuwa uhusiano baina ya Marekani na Urusi kuboreka .

 Habari Zinazohusiana