Je, ni mwaka mpya wa sura mpya kwa Syria?

Je, ni mwaka mpya wa sura mpya kwa Syria?

Je, ni mwaka mpya wa sura mpya kwa Syria?

Imebakia wiki mbili pekee kabla ya Donald Trump kuchukua usukani wa kuwa rais mwengine wa Marekani.

Uongozi wake uankuja wakati ambapo matukio na makundi ya kigaidi yameongezeka kote ulimwenguni.Ni wazi kuwa majina ya makundi haya ya kigaidi yanatofautiana lakini matendo na malengo yao ni sawa .Hivyo bas ini sahihi kusema kuwa makundi haya ya kigaidi yanongozwa na kupata fikra kutoka kwa kiongozi mmoja .

Rais wa Ufaransa amekosoa sera za Erdoğan za kurudisha usalama na ustawi nchini Syria,na wakati huo huo Nchini Ufaransa miji mingi ya kitalii ikiwa ni pamoja na Paris ilianza kuvamiwa namagaidi na kusababisha vifo na umwagikaji wa damu kwa raia na maaelfu ya watalii.Hii ni kwa sababu Ufaransa kwa muda wa mwaka mmoja imekuwa inaongozwa na utawala  maalum kwa jina la ‘Hali bora zaidi’.

Ufaransa ni nchi inayotambulika ulimwenguni kuwa mfano bora zaidi katika mifumo ya kidemokrasia na uhuru na haki za raia wake lakini cha kushangaza kuwa imewacha maamuzi ya kisiasa kufanywa na mahakama hata ikiwa ni masuala ya mapambano dhidi ya ugaidi.,

Huku Rais Erdoğan akihimiza umuhimu wa kuzingatia amani,utulivu na haki za kibinadamu nchini Syria serikali ya kansela wa Ujerumani Merkel ilikumbwa na mashambulişzi mabaya ya ugaidi na kusababisha mauaji mengi.

Kwa sasa ni dhahiri kuwa sera za Erdoğan zinazosisitiza umuhimu wa kuleta ustawi nchini Syria zinapingwa na kupuuzwa na viongozi wengi wa magharibi.Viongozi wengi wa Magharibi na EU wamekaa kimya na kuunga mkono sera za Obama ambazo zimepelekea umwagikaji mwingi wa damu dunaini.

Rais Obama alisisitiza umwagikaji wa damu nchini Syria na pia kuendeleza sera hiyo kote duniani.Utawala wa Iran kwa muda mrefu unaonekana kuwa adau mkubwa kwa Marekani,lakini ilionekana kuwa kama utani mkubwa baada ya kuitetea Marekani na sera zake.

Bila shaka Uturuki inafanya juhudi zote ili kuhakikisha kuwa hadhi na usatawikatika nchi ya Syria unaimarshwa na kurudi kama zamani.Uturuki kwa sasa haina huruma wala kusamehe kundilolote la kigaidi nchini Syria nah ii ndiyo sababu imekuwa ikifanya operesheni dhidi ya makundi haya nchini Syria .

Kwa kweli limekuwa jambo ghali zaidi sasa kutaka kupna Syria yenye amani na uhuru kipindi hiki.Hivi karbuni Uturuki imevamiwa na magaidi kama PKK/PYD na DAESH katika mashambulizi yaliyopelekea mauaji ya raia,polisi na askari .

Ni jambo pia la kuzua maswali mengi kuwa baada ya mashambulizi haya ulimwengu wa magharibi hutuma kwa haraka salamu za rambi rambi kwa Uturuki na kuatoa ahadi kushirikiana na Uturuki katika mapambano dhidi ya ugaidi lakini Uturuki ikipiga hatua ya kuingia Syria na kuwapiga vita magaidi nchini humo huachwa katika mapambano haya peke yake .

Marekani,NATO na EU imeiwacha Uturuki peke yake wakati jeshi la Uturuki lililpoingia nchini Syria .

Licha ya kuwa mashirika haya yanayojidai kuwa rafiki wa Uturuki kutotoa msaada wowte kwa Uturuki katika mapambano ,Uturuki imejikakamua na kufanikiwa kuingia Syria .Kwa takriban miaka 4 tangu mashirika haya kutangaza kuwa wanapambana na DESH nchini Syria hakuna mafanikio yoyote yaliobainika .Lakini kwa upande wa Uturuki,ni siku zisizozidi mia 2  na tayari wammeweza kuwaondoa na kuwauawa magaidi wa PYD na DAESH nchini humo.Hii ni katika hali ya kwamba Marekanipia haijatoa mfumo wao wa kufanya udadisi kutoka angani.

Baada ya kuonekana kuwa kuna mafanikio ya juhudi za Uturuki katika mapambano dhidi ya makundi haya ya kigaidi sasa mashambulizi ya kila aina kutoka PKK,PYD na DAESH yameendelezwa katika miji mikuu ya nchi ya Uturuki.Maelfu ya Askari,polisi na raia wasio na hatia wameuawa .

Kama ilivyo destur ini kuwa mashambulizi haya yanayotekelezwa nchi Uturuki hulaaniwa na mataifa haya ya magharibi na kutuma slamu za pole pekee kwa Uturuki.

Baada ya shambuliz katika klabu usiku wa kuukaribisha mwaka mpya jijini Istanbul lilitekelezwa na DAESH ,Magharibi ilionyesha harakati za kustaajabisha .Katika makao makuu ya NATO bendera ya Uturuki ilipeperushwa nusu mlingoti na kutangaza kuwa ipo pamoja na Uturuki.Hil, ni jambo la kushangaza kwa sababu hadi hivi leo haman hata siku NATO imeungana na Uturuki kupambana na makundi ya kigaidi kama DAESH,PKK na PYD.Hii ina maana ya wazi kuwa NATO haihuzunishwi na mauaj, ya halaiki ya watu bali inatumia tu sera za kisiasa kuonyesha mchango wake katika suala hili.

Hatua kubwa ambayo NATO imeweza kuchukua ni kupeperusha bendera ya Uturuki nusu mlingoti.

NATO ni shirika la usalama ambalo lina uanachama na Uturuki na jambo la sahihi kufanya zaidi ni kushirikiana na Uturuki kulinda usalama wa askari wake na raia wa Uturuki lakini imechagua kupeperusha bendera ya Uturuki nusu mlingoti.

Ni wazi kuwa NATO haijali usalama wa raia wa askari wa Uturuki bali huchukua hatua za kisiasa .

 

 

 Habari Zinazohusiana