Al Bab,changamoto kuu katika operesheni ya Fırat nchini Syria

Al Bab,changamoto kuu katika operesheni ya Fırat nchini Syria

Al Bab,changamoto kuu katika operesheni ya Fırat nchini Syria

Kuna uwezekano kuwa watu wengi ambao hawaishi Syria na maeneo jirani kutotambua au kutojua operesheni ya Fırat .Wiki hii katika kipindi chetu cha Mtazamo wa Uturuki kwa mashariki ya Kati tutachambua matukio ya operesheni inayoendelea ya Fırat Kalkanı katika eneo la Al Bab nchini Syria.

Kutoka chuo kikuu cha Atatürk kitengo cha Utafiti wa uhusiano wa kimataifa Dkt prof Cemil Doğaç İpek anatoa tathmini ya kipindi chetu cha leo.

Serikali ya Jamhuri ya Uturuki kwa muda mrefu imekuwa ikifanya juhudu katika mapambano dhidi ya makundi ya kigaidi kama DAESH,PYD,PKK na FETÖ.Licha ya kuwa na changamoto mbali mbali operesheni ya Fırat Kalkanı nchini Syria inaendelea kwa mafanikio.Kwa muda wa siku kumi katika eneo la Çobanbey karibu na Jarablus jeshi la Uturuki liliweza kuteka maeneo ya Dabık ambayo yalikuwa maeneo muhimu sana kwa kundi la kigaidi la DAESH.Ushindi huu ulipelekea matumaini wa kuweza kuwaondoa magaidi hao katika maeneo ya Al Bab .

Hata hivyo ni wazi kuwa kufanikiwa katika kuwaondoa magaidi hao Al Bab si kazi rahisi.Hii ni kwa sababu idadi ya magaidi hao ni kubwa kuliko hata maeneo ya Dabık,Jarablus na Çobanbey.Hata hivyo jeshi la Uturuki liliendelea na kuzingira Al Bab kutoka kwa maeneo 6 ya kanda hiyo.Hivi sasa jeshi la Uturuki,Jeshi huru la Syria wakishirikiana na muungano wa Waturkmeni wameungana katika kufanikisha operesheni dhidi ya DAESH maeneo ya Al Bab .

Kulingana na maelezo tuliyoyatoa juma lililopita,operesheni katika eneohiyo inafanywa kwa uangalifu ili kuzuia uharibu wa makaazi ya watu pamoja na pia ni msimu wa baridi kali katika kanda hiyo.Pia makundi ya PKK,PYD na DAESH katika kanda hiyo wanaonyesha upinzani kwa mara kumi zaidi.DAESH mbali na kuwa wanapata msaada kutoka kwa nguvu za juu za magharibi pia wamesimamisha utawala wa Assad jambo ambalo linaipa nguvu zaidi.

Muungano huo ulio na uhusiano na Marekani pia uliweza kusimamisha operesheni ya Mosul hapo awali.Hivi sasa ni Uturuki pekee inayopambana dhidi ya DAESH katika eneo pekee lililobakia katika operesheni hiyo ,eneo la Al Bab.Ni jambo la kushangza kuwa wakati kama huu ambapo Uturuki inawapoteza majeshi wake katika operesheni hiyo na baadhi ya wanahabari na vyombo vya habari vimeanzisha uvumi kuwa Uturuki na DAESH wanafanya ushirikiano ,kusema kweli wanafaa kuomba msamaha kwa Uturuki.Inakadiriwa kuwandani ya Al Bab kunapatikana takriban magaidi 300 wa kujitoa mhanga .mbali na hapo magaidi hao wanatumia raia kama kinga wao dhidi ya jeshi .

Mbali na kuwa na changamoto hizi bado jeshi la Uturuki na Jeshi huru la Syria lina maatumaini na nguvu ya kuikomboa Al Bab.Ikiwa jeshi huru la Syria linaloungwa mkono na Uturuki litashinda kuikomboa Al Bab basi magaidi wa DAESH walio kanda ya Mashariki mwa Syria watakuwa wasio na nguvu tena .Kuna matumaini kuwa baada ya ushindi huu serikali mpya katika kanda ya kaskazini mwa Syria kuundwa.Uturuki na jeshi huru la Syria itaipa nguvu maeneo ya Munbich,Al Bab,Raqqa na Afrin .Hivyo basi Uturuki itakuwa na nguvu katika kuleta suluhu ya kisiasa nchini Syria.

Baada ya jeshi huru la Syria kuweza kuweka udhibiti katika Al Bab kuna uwezekano ya mambo mawili kutokea .

Kwanza kabisa kuna uwezekano jeshi la Syria litaongoza maeneo ya Afrin na Munbinch ama pia uwezekano wa Jeshi la Syria kupigana na PKK na PYD NA baadaye mchakato wa mpango mpya wa kisiasa kuaanzishwa .

Kuna matumaini pia kuwa Uturuki na Marekani kuungana na kufanya operesheni ya pamoja Raqqa.

Maana kamili ya Al Bab ni mlango.Pengine milango ya nchi zingine itafunguka huku zingine milango yao kufungika .Kwa sasa hamna lolotee lililobainika lakini labda baada ya Donald Trump kuingia uongozini Januari 20 mambo yatakuwa wazi zaidi.

 Habari Zinazohusiana