Uhaba wa maji nchini Syria

Hatua za kutengeneza tena mfumo wa maji jijini Sham zaanzishwa

Uhaba wa maji nchini Syria

Uhaba wa maji wakumba maeneo mengi nchini Syria baada ya vita vya ndani.

Hata hvyo hatua zimeanza kuchukuliwa jijini Sham kutatua uhaba huo wa maji .

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa ni kuwa wakaazi wa vitongoji 12 jijini Sham wamekubali wito wa Assad wa  kuondolewa katik eneo la bonde la Barada .

Baadhi ya wapiganaji wapinzani pia wameanza kuondoka eneo hilo .

Hata hivyo wapinzani 60 wameripotiwa kuondoka eneo hilo huku wengine akikataa kuondoka eneo la bonde hilo .

Baadhi ya wakaazi pia wamefahamisha kuwa kulikuwa na mvutano baina ya wapizani hao .

Hata hivyo utawala wa Assad umeahidi kutengeneza mifumo ya maji eneo la Barada baada ya watu kuondoka eneo hilo .

Bonde la Barada ni eneo muhimu la asili ya maji ya jiji la Sham .

Pia habari zafahamisha kuwa utawala wa Assad bado unashambulia maeneo ya wapinzani kwa mashambulizi ya angani.

Maeneo haya ni pamoja na Guta ya Mashariki,Kusini mwa Aleppo na Idlib.

 

 Habari Zinazohusiana