Uturuki na mtazamo wa Mashariki ya Kati

Uturuki na mtazamo wa Mashariki ya Kati

Uturuki na mtazamo wa Mashariki ya Kati

 

Licha ya vikwazo vyote, Serikali ya jimbo la waukrdi la Iraq ya Kaskazini ilipiga kura ya maoni ya kujitenga na Iraq. Kufuatia kura ya maoni hiyo kinume na sheria za kimataifa, serikali ya Iraq iliingilia kati ya na serekali yajimbo la  wakurdi wa Iraq ilianza kujiondoa na kurejea kwenye mipaka ya 2003. Ingawa serekali ya jimbo hilo iliwania uhuru, lakini kura  hiyo imeidhoofisha na kusalimu amri ya serekali ya Baghdad.

Kura hiyo ya maoni  ilianzisha mabadiliko makubwa nchini Iraq. Jeshi la Iraq lilichukua maamuzi ya haraka likishirikiana  na Iran, na Uturuki ili kuzima mpanga wao . Kirkuk na maeneo yenye utata walirudi kwenye mikono ya serekali kuu ya Iraq. Udhibiti wa mipaka na viwanja vya ndege vilirudi kwenye mamlaka za Baghdad. Jeshi la Iraq limetia ngome zake  kwenya mpaka wa Habur. Mpaka wa Syria na Iraq pia umedhibitiwa tena na serikali ya Baghdad.  Uturuki na Iran, ambazo walikuwa na utofauti wa sera na mtazamo kuhusu vita ya Syria, mgogoro wa jimbo la wakurdi la Iraq iliwasogeza karibu na kuiunga mkono serekali ya Baghdad dhidi ya Erbil.

Wakati huo huo, serekali ya jimbo la wakurdi la Iraq haikuwa tu na matarajio ya uhuru, lakini pia imeshindwa mradi wake  dhidi ya Katiba ya 2005. Kwanza ilipoteza utawala wake mkoani Kirkuk, na baadaye ikapoteza udhibiti wake wa rasilimali. Pamoja na maendeleo ya hivi karibuni, serekali ya Erbil ilipoteza faida muhimu ya uchumi, na kuifanya pia serekali ya Baghdad kuwa na nguvu zaidi. Pigo walilopata kiuchumi ni kupoteza visima vya mafuta kwenye maeneo ya mzozo kati ya Baghdad na Erbil. Serikali ya Iraq inataka kupata udhibiti kamili wa mipaka yake yote. Udhibiti wa mipaka ni angalau kwa serekali ya Erbil kuliko  kupoteza mapato ya mafuta, ambao  imekuwa ikijipatia tonge nono kutoka uzalishaji wa mafuta tangu miaka ya 1990.

Ushirikiano wa Uturuki, Iran na Iraq, kwanza kabisa, uliangamiza kwa urahisi jitihada za majeshi yanaoungwa mkono na serekali ya Erbil. Kipengele 140 cha Katiba ya Iraq, kilichoacha wazi kuhusu utawala wa Kirkuk na maeneo yanaozozaniwa huenda kikatupiliwa mbali na Baghdad ili kuzuia tena Erbil kurudi katika maeneo hayo.

Utafiti unaonesha kuwa Erbil itakapotaka tena kurudi katika maeneo ya mzozo na Baghad, hii itapelekea kuzuka kwa mgogoro mkubwa kabisa ambao unaweza kupelekea hata serekali ya Erbil kusambaratika.

Mnamo mwezi wa Novemba, Iraq imeingia katika kipindi cha zama mpya kwenye historia yake. Huenda kipindi cha takriban miaka 14 ya kukaliwa na Erbil kikafika mwisho, na Iraq kujipatia uhuru wake kamili.

Utambulisho wa kitaifa wa Iraki, ambao umeundwa na umoja wa makabila na imani tofauti umeimarika baada ya Erbil kujitenga. Wasuni, washia na waturkmen walioshirikiana bega kwa bega katika vita ya Hasidi Shabi dhidi ya Erbil waliongozwa na kamanda wa kikurdi wa jeshi la Iraq. Uchaguzi wa mwaka kesho Iraq bila shaka utakuwa unatawaliwa na tukio hili. Kama waziri mkuu wa Iraq wa sasa atajinyakulia ushindi, basi itakuwa ni hatua kubwa mhimu kuelekea umoja wa Iraq. Sababu Uturuki, Iran, na Iran  huhitaji umoja huo.

Kuna uwezekano mkubwa wa kupiga hatua na kuimarisha uhusiano baina ya Uturuki na Iraq katika siku za usoni. Kwa sababu Uturuki iliisaidia Iraq kikamilifu  na kuirudisha Iraq kwenye hali ya kujitegemea. Ushirikiano kati ya nchi hizo mbili, utajikita hasa katika vita dhidi ya ugaidi.Iraq inaitegemea sana Uturuki kuisaidia kufyeka kundi la PKK na DAESH nchini Iraq.

 Habari Zinazohusiana