Uturuki na mtazamo wa Mashariki ya Kati

Uturuki na mtazamo wa Mashariki ya Kati, Lebanon

Uturuki na mtazamo wa Mashariki ya Kati

 

Viongozi zaidi ya 30, ikiwa ni pamoja na wana mfalme 11, walikamatwa na kufungwa nchini Saudi Arabia. Kwa upande mwingine, Waziri Mkuu wa Lebanon Saad Hariri alijiuzulu alipokuwa ziarani huko Riyadh. Hariri ameishutumu Iran kuchochea vurugu kwa kutumia kundi la Hezbollah nchini Lebanon . Kwa kweli, ni jambo la kushangaza kwamba Hariri aliekuwa akishikilia wadhifa wa waziri mkuu akishirikiana na Hezbollah na leo atangaze wazi kuwa Hizbollah na Iran wanapanga njama za kuyumbisha amani Lebnanon . Tukio hili linadhihirisha madai ya Hezbollah kuwa Hariri alijiuzulu kwa uamuzi wa Saudi Arabia". Kila mtu anaefuatilia kwa karibu migogoro na siasa za Mashariki ya kati, hujiuliza maswali mengi.

 Kwa mujibu wa muundo wa siasa uliotengenezwa na wafaransa miaka ya 1930, rais anachaguliwa kutoka jamii ya wakristo, waziri mkuu hutoka jamii ya waislamu wa Sunni, na spika wa bunge hutoka waislamu wa Shia. Mfumo huu wa kisiasa wa Lebanoni hufanya nchi za kigeni kuweza kuingilia mambo ya Lebnon. Kwa sababu hii, baadhi ya nchi za Magharibi, Saudi Arabia na Iran zinaweza kuingilia kati katika muundo wa ndani wa Lebanon. Iran ikianza kutumia Hezbollah kama daraja la ushawishi wake, basi Saudi Arabia nayo inajaribu kuingia Lebnon kwa kutumia familia ya Hariri.

Lebanoni haikujali sana wakati kanda nzima ilikuwa inajishughulisha na mgogoro wa Syria. Wale wanaoishi Syria walisaidia kuongeza ushawishi wa Iran katika kanda. Hezbollah ni mfano wa waenezaji wa ushawishi wa Iran nchini Syria na Lebanoni. Israeli imeridhishwa sana na hali inaofanya Hezbollah kushughulika sana na mgogoro wa Syria. Lakini kwa upande mwingine wa Israeli, shida ni kwamba wale wanaoishi Syria wameiimarisha zaidi Hezbollah. Israeli inapata vitisho kutoka maelfu ya wanamgambo wa Hezbollah wanao ongozwa na Iran nchini Syria.

Kuna wale ambao wanatathmini mabadiliko Saudi Arabia kwa upande wa siasa za ndani na uchumi. Kulingana na tathmini hizi, Saudi Arabia; Iran na Hezbollah wanatumia lugha ya chini kwa chini kuchochea vurugu. Lakini vitisho vya vita vya Saudi Arabia dhidi ya Lebanoni havina umuhimu wowote wa kuonesha kuwa Muhammad bin Salman ana nguvu kwenye kanda au laa. Sera ambayo Saudi Arabia inaendesha huko Qatar, Yemen na Syria zinaonyesha bila shaka kwamba Saudia Arabia wanaweza kuchochea hata kutumia nguvu na kuonesha nguvu zao Mashariki ya Kati.

Uturuki inaangalia mgogoro wa kamata kamata unaoikumba Saudi Arabia kama jambo la ndani la Saudi Arabia. Kwa upande mwingine, Saudi Arabia haikurekebisha uhusiano wake na Ankara baada ya mgogoro wa Qatar na msaada wake kwa kura ya maoni nchini Iraq. Inawezekana, nchi zote mbili zinadhani kinachoendelea Lebanoni hakitaharibu mahusiano yao moja kwa moja.

Mgongano nchini Lebanoni husababisha Hezbollah kupungua uwepo wake Syria. Hii inadhoofisha utawala wa Asad. Hezbollah kujiondoa Syria huongeza uwepo wa Uturuki nchini Syria. Hali hii inaweza kuimaraisha vita vya Uturuki dhidi ya kundi la kigaidi la PKK / YPG. Itakuwa vigumu sana kwa Marekani na washirika wake kuingilia kati dhidi ya operesheni za Uturuki kupambana na PKK / YPG nchini Syria. Aidha, Iran na Urusi zinaweza kuhitaji uwepo wa Uturuki nchini Syria. Lakini ikiwa Saudi Arabia itaendelea na mgogoro wake na Qatar badala ya Lebanoni, hali hii italeta tena mvutano baina ya Uturuki na Saudi Arabia.

Mchakato ulioanza kama kupambana na rushwa nchini Saudi Arabia na kujiuzulu kwa Hariri huenda ukachukua mkondo mwingine katika Mashariki ya Kati. Uhai ni ngumu sana kwamba unaweza kuelezewa tu na mabadiliko ya nguvu nchini Saudi Arabia.

Mabadiliko nchini Saudi Arabia yanaweza kuleta sura na mazingira ya vita katika Mashariki ya Kati. Katika hali hiyo, Uturuki itaathirika. Kutokana na uwepo wa waturkmen nchini Lebanoni, wanadiplomasia wa Uturuki itawabidi kunyamanza na kutoegamia upande wowote katika mgogoro wa Lebanon. Matokeo ya mgogoro huu pia huweza kuathiri masilahi ya Uturuki.

 

 Habari Zinazohusiana