Uchambuzi wa matukio

Mchezo wa kuigiza wa Daesh

Uchambuzi wa matukio

Kwa kipindi cha miaka mingi tuliweza kufahamisha kuwa kundi la kigaidi la wangambo wa Daesh halina uhusiano wowote wa kikanda. Ila kwa vyovyote vile wataalamu  katika katikas suala la ugaidi hawakuweza kuaminiwa kwa kile walicho fahamisha kuhusu kundi hilo.  Na haswa  kupitia vyombo vya habari vya Magharibi,  hawakuweza kuamini hilo kuwa kundi la Daesh halina uhusiano wa kikanda. Wapo wale ambao walitamka wazi kuwa hawawezi kuamini hivyo.

Mawakili na washirika waliokuwa na umuhimu mkubwa walikuwa huru na saula hilo.  Baadhi yao walikutana na waandishi wa habari na mitandao ya kijamii waliweza kuandaa mikutano  ya kimataifa baada ya kutahadharishwa kutokana na ushirikiano uliokuepo.

Ushirikiano wetu ulikuwa katika mstari wa mbele. Kujitenga na kujigawa kwa Yugoslavia, vita vya Rwanda vya wenyewe kwa wenyewe. Tuliweza kuunda urafiki na Afrika kutokana na matukio tofauti ambapo pia kulikuwemo matukio ambayo hayakuwa ya kuridhisha na vita kadhaa katika ukanda wa Mashariki ya Kati.

Marafiki zetu waliokuwa wakiishi katika sehem moja walijikuta wamekuwa maadui ila baada ya muda walijikuta wakiwa chini ya mwavuli mmoja.

Baada ya muda wale ambao waliona ubaya na ukweli kuhusu kundi la wangambo wa Daesh hawakuweza kutoa taarifa yeyote iliowahusu katika vyombo vya habar.

Kundi la kigaidi la Daesh lilifahamika kwa mashambulizi na uharibifu wake na kuzoeleka. Mbinu walizotumia wanamgambo wa kundi hilo ziliweza ktafsiriwa na wadadisi kuwa  mbinu za baadhi ya mataifa washirika wa NATO. Suala hilo liliweza kusumbua vichwa katika kipindi cha miaka kadhaa na jibu lake liliweza kuonekana katika uchaguzi mkuu nchini Marekani.

Katika ukurasa wake wa twitter mgombea kiti cha urais Donaşd Trump wakati huo aliandika  kuwa Obama amenzisha kundi la Daesh na baadae alifuta ujumbe wake huo.

Baada ya Trump kufanya hivyo, magharibi kulionekana kuzaliwa upya ushirikiano na Magharibi.

 

Tutazame kwa ufupi takwimu zinazo onesha operesheni za kijeshi zilizoendeshwa na Marekani  dhidi ya Daesh:

Idadi ya mashambulizi ya anga dhidi ya Daesh na jeshi la ushirika : 28181

Kiwango cha siku za mashambulizi 1185

Wanajeshi walishindwa kumudu na wangambo : 5000

Idadi ya mabomu na makombora yaliotumiwa dhidi ya Daesh: 102082

 

Ukitazama takwimu hiyo kwa umakini utaona na kubaini kuwa ni mchezo uliowazi. Jeshi la ushirikiano na Marekani  halina ukweli katika idaidi ya wanajeshi ambao wametumwa katilka vikosi maalumu katika kupambana na wangambo wa kundi la Daesh.  Tunaweza kufahamisha kundi la kigaidi la PYD ambalo ni tawi la kundi lingine la kigaidi n a mshirika wa Marekani linaweza kuwa na zaidi ya wanamgambo 100 000 nakutoa taarifa kuhusu jeshi.

Siku chache zilizopita tumeona katika kituo cha habari cha Uingereza BBC kikipeperusha picha mabazo zinaonesha ushirikiano uliowazi wa wangambo wa Daesh na Marekani. Kila kinachotambulika wazi ni kuwa sula hilo halikuzungumziwa kama ilivyo kawaida katika vyombo vya habari Magharibi. Hakuna yeyote alionekana kuhudi tukio hilo. Jambo lingine la kushangaza na mataifa ambayo tayari yalikwisha shambuliwa na wangambo wa kundi la kigaidi la Daesh nayo yalisalia kimya. Hapo tunazungumzia mataifa ya Umoja wa Ulaya ambayo raia wake waliuawa katika mashambulizi na wangambo wa Daesh.

Uturuki na nguvu zake za kşjeshi iliweza kuwaondoa wangambo wa kundi hilo la kigaidi katika mipaka yake baada ya kusababishiwa hasar ana kundi hilo. Wnajeshi 300 waliweza kuwaondoa wanamgambo hao waliokuwa wakitishia usalama wa Uturuki katika mipaka yake. Vitisho vya wanagambo hao vimetolewa moja kwa moja katika mipaka ya Uturuki.

Kwa muda wa miezi miwili jeshi la Uturuki liliweza kuwaondoa  wanamgambo hao ambao Magharibi imetumia zaidi ya miaka bila ya kufaanikiwa. Wanajeshi 500 katika operesheni hawakusaidiwa kwa operehsni za anga dhidi ya Daesh. Kwa muda wa zaidi ya miaka minne jeshi la ushirikiano lilitumia silaha nzito dhiiiiiidi ya Daesh bila ya kufaulu.

Mapambano dhidi ya ugaidi  yanayoendeshwa na Marekani ni suala ambalo wanatakiwa waandishi wa habari kuhoji na kujadili suala hilo.

Uturuki, Urusi, Uingereza, Iran na Syria zinatakiwa  kuwa na mfumo wa sheria ya kimataifa kwa pamoja.  Mamia ya watu wamepoteza maisha wakiwemo watoto, wamawake kutokana na uhalifu wa kundi hilo. Mashaka ambayo yanajitokeza kuhusu kundi hilo yanatakiwa kufikishwa katika vyombo husika vya kimataifa. Iwapo suala hilo halito zungumziwa basi uongozi ulimwenguni na mfumo mpya wa utawale utakuwa bado ni suala lisilopatiwa ufumbuzi.

Kundi la kigaidi la wahaini wa FETÖ katika miaka ya nyuma limetetewa kuwa sio kundi la kigaidi.

M agharibi imefumbia macho madai ya Uturuki kuhusu kundi hilo na kufikia hadi kutoa uraia na hati za kusafiria kwa watu ambao walihusika katika jaribio la mapinduzi Uturuki. Ni wazi kuwa kuna njama dhidi ya Uturuki.

 Tunaweza kuuliza kuwa ni nani ambae hataki kuna maigizo hayo hayafiki mwisho?


Tagi: Deash

Habari Zinazohusiana