Msaada wa Uturuki kwa jamii ya Rohingya Bangladesh

Recep Akdağ Naibu waziri  mkuu wa Uturuki asema kuwa  uturuki itafungua hospitali 2 kwa ajili ya rohingya nchini Bangladesh

Msaada  wa Uturuki kwa jamii ya Rohingya Bangladesh

Recep Akdağ  akumbusha kuwa Cox Bazar nchini Bangladesh imepokea wakimbizi wa jamii ya Rohingya kutoka takriba watu milioni moja kutoka Myanmar.

Naibu waziri mkuu wa Uturuki amesema kuwa Uturuki itaweka hospitali mbili katika eneo hilo kwa ajili ya wakimbizi wa jamii ya Rohingya waliokimbia Myanmar.

Waziri wa Bangladesh anaehusika na uongozi wa kitengo kinachohusika na ugawaji wa misaada Mustafa Hussen alipokelewa  mjini Ankara Jumanne na naibu waziri mkuu wa Uturuki.

Katika mkutano wao huo, alishiriki pia Mehmet Gülluoğlu ambae ni mkurugenzi wa shirika la misaada la Uturuki AFAD.

Mkurugenzi wa AFAD amesema kuwa kabla ya mwaka 2017 kumalizika Uturuki itaweka hospitali mbili Cox Bazar kwa ajili ya kutoa matibabu kwa waambo hifadhi na wakimbizi kutoka Myanmar.

 Habari Zinazohusiana