"Kombora hilo ni tishio kwa ulimwengu mzima"

Korea Kaskzini yajaribu kombora kwa mafaanikio na kusema kuwa inoa uwezo wa kufika   Marekani

"Kombora hilo ni tishio kwa ulimwengu mzima"

 

Korea Kaskazini imejaribu kwa mara nyingine kombora lake la masafa marefu na kusema kuwa kwa sasa makombora kutoka Korea yanaweza kufika katika ardhi ya Marekani.

Kituo cha runinga cha taifa KNCA  kimefahamisha kuwa kombora aina ya Hwasong-15 limejaribiwa kwa mafaanikio.

Rais Kim Jong-Un  amesema kuwa  Korea inayo furaha kuweza kutimizza ndoto zake za kihistoria  kuwa na nguvu za nyuklia.

Waziri wa ulinzi wa Marekani James Mattis amesema kuwa kombora hilo ni tishio kwa ulimwengu mzima.

Rob Manning, msemaji wa idara ya ulinzi amefahamisha kuwa kombora hilo baada ya kusafiri kwa umbali wa kilomita  1 000 limeanguka katika bahari ya Japani.Habari Zinazohusiana