"Walemavu wanapashwa kujifunza kuishi kwa kujitegemea"

Mwanamichezo mlemavu wa Uturuki amewashauri walemavu wote kujitahidi kuishi maisha yao kwa kujitegemea bila kusubiri msaada kutoka kwa wazazi.

"Walemavu wanapashwa kujifunza kuishi kwa kujitegemea"

Mwanamichezo mlemavu wa Uturuki amewashauri walemavu wote kujitahidi kuishi maisha yao kwa kujitegemea bila kusubiri msaada kutoka kwa wazazi.

Siku ya Jumapili 3.12.2017,dunia imesherehekea siku ya walemavu duniani,siku ambayo ilitambuliwa na Umoja wa Mataifa mwaka 1992.

Abdullah Öztürk ambae ni mwanamichezo mlemavu wa Uturuki alishinda medali ya dhahabu katika mashindano ya tenisi mwaka 2016 nchini Brazil.

Kwa mujibu wa habari,kwa sasa Öztürk ni kocha wa walemavu na amekuwa akishawishi walemavu na kuwapa moyo wa kuishi kwa kujitegemea.

Mwanamichezo huyo mwenye umri wa miaka 28,amejizatiti maisha yake katika michezo na kusema kuwa ni jambo muhimu sana katika maisha yake.

Öztürk amewataka walemavu wote kamwe kutokata tamaa.

 Habari Zinazohusiana