Uturuki na Saudi Arabia kudumisha mahusiano katika sekta ya afya

Uturuki na Saudi Arabia zinatarajia kudumisha uhusiano wao katika sekta ya afya.

Uturuki na Saudi Arabia kudumisha mahusiano katika sekta ya afya

Uturuki na Saudi Arabia zinatarajia kudumisha uhusiano wao katika sekta ya afya.

Waziri wa afya wa Uturuki Ahmet Demircan amekutana na waziri wa afya wa Saudi Arabia Tawfik bin Fawzan Al Rabiah katika mkutano wa mawaziri wa afya ulioandaliwa na OIC.

Waziri wa Uturuki amesema kuwa anaamini kuwa nchi yake inaweza kufungua na kuongoza hospitali nchini Saudi Arabia na hata ikiwezekana mjini Mecca.

Waziri huyo vilevile amewahamasisha wafanyabiashara kushirikiana katika utengenezaji wa vifaa vya hospitali na makampuni ya Uturuki.

Waziri wa Saudi Arabia kwa upande wake amesema kuwa nchi yake iko katika hatua ya kubinafsisha mahospitali.

Mpaka sasa Saudi Arabia ina hospitali 270.

 Habari Zinazohusiana