Mtazamo

Waislamu jamii ya Rohingya, Rakhine au damu tupu

Mtazamo

 

 

Labda hadi kufikia sasa hakuna mabadiliko makubwa, waislamu jamii ya Rohingya walijipata katika matatizo makubwa  baada ya Agosti 25 mwaka 2017 walipojaribu kunusuru nafsi zao kutokana na mauaji na unyanyasaji waliotendewa na uongozi wa Myanmar. Watu 500 000 walilazimika kuondoka katika eneo hilo na kukimbilia nchini Bangladesh kutafuta hifadhi. İlikuwa ni ambayo ni ya kusitikisha na kutia ghofu kubwa kutokana na mauaji yaliokuwa ya kinyama.

Kipindi chetu cha leo kimetaarishwa ba profesa Kudret Bülbül kutoka katika chuo kikuu cha Yıldırım mjini Ankara.

Tuanze na kuizungumzia Maynmar kijiegrafia kabla ya kuingi a moja kwa moja katika kipindi chetu, Myanmar ni taifa ambalo linapakana  Thailand, Laos, China, India, Bangladesh  na Ghuba ya Bengali.  Rakhine ni eneo ambalo lipo kimkakati kutoka na eneo ambalo inapatikana, kwa kifupi ni eneo muhimu katika eneo hilo kwa kuwa linapatikana kando kando ya bahari.

Rakhine ni eneo ambalo wafanya biashara wa kiislamu walikuwepo hapo kwa muda mrefu wakisafiri katika kuendesha baishara zao katika ghuba ya Bengali.

Wailsmu wa Rakhine kama waislamu wa Moro wanaishi katika eneo hilo kwa kipinidi kwa karne kadhaa  katika uongozi ambao uliokuwa chini ya himaya yao. Mwaka 1885 eneo hilo lilikaliwa kimababvu na Uingereza katika zoezi lake la kueneza ubabe kama ilivyofanyika katika maeneo mengine ulimwenguni.

Baada ya kupambana na Uingereza Myanmar ilijipatia uhuru wake  mwaka 1948, mwaka 1962 kamanda NE Win  aliingia madarakani baada ya kupindua serikali mwaka 1962 na kubadilisha jina la nchi kutoka Burma na kuwa  Myanmar.

 Katika kipindi cha utawala wake waislamu waliishi katika ardhi hiyo walikuwa wakilazimishwa kuondoka katika majumba yao. Walikuwa wakishambuliwa na wabuddha.

Katika miaka ya nyuma madhila yalizidi kuongezeka kwa jamii ya waislmu hao  ambao walilalzimika kukimbilia ukamisho, umwagaji damu kwa lugha ya Kituruki Arakan tunaweza kusema kuwa ni Anakan ikiwa na maana chanzo cha damu kumwagika.

Uongozi wa jamii ya Rohingay barani Ulaya  na naibu wake msaidizi wamezungumzia suala la madhila ya wjamii ya  Rohingya na kila kinachoendelea. Ushirikiano wa balozi  Ümit Yardım walianzisha jukwaa katika chuo kikuu cha Yıldırım Beyazit  amblao halina lengo la kujipatia pesa.  Tuliuliza kuhusu  matukio hayo . La Jo, na Muhammed Hubeyb katika kutafu  usalama na kuondoa ubaguzi na picha ambayo ilikuwa ikionekana

Iwapo kuna uwezekano wakufikia katika matumiani tunaweza kuzungumzia kuhusu ufumbuzi.

 

  1. Katika kukabiliana na seriakli ya Myanmar, jumuiya ya kiğmataifa inatambua kuwa kilichotendekea Myanmar katika jimbo la Rakhine ni kinyume na haki za binadamu, unyama na unyanyasaji huo unatakiwa kukomeshwa kwa hali yeyote ikibidi iwapo diplomasia itakwama nguvu na vikwazo vitumike. Mashirika ya kimataifa ya kutetea  haki za binadamu yasimame katika wajibu wake. 

  2. Katika kutafuta ufumbuzi kwa ushirikiano wa kimataifa  kuntakiwa kuundwa tume kama ilivyofanyika  nchini Ukraina katika mzozo ulioibuka. Mashirika ya kimataifa yalijiunga na kuunda tume tofauti ili kufikia katika hali iliokuwa ikiridhisha pande zote mbili na kutatua mzozo uliokuwepo. China na India ni mataifa ambayo tunatambua vema kuwa ni miongoni mwa mataifa mbayo msimamo wao hua hunaathari kubwa  katika kutatua tatizo.  Ni vema kushirikisha mataifa hayo kwa kuwa ni jambo ambalo linawezekana na muhimu. Wajibu wa makundi ambayo yataundwa katika kutafuta ufumbuzi huo ni ni kuhakikisha kuwa jamii ya Rohingya inakuwa katika hali nzuri na salama. Vile vile jamii hiyo kurejea katika ardhi yao na kutendewa haki na kuishi kwa amani.   

  3. Katika kuzuia hali isioridhisha kutokana  na unyanyasaji, udhalimu na ukiukwaji wa haki wanaotendewa jamii ya Rohingya ni kama jamii ya wakudri nchini Syria ambao pia hawatambuliki na kunyanyaswa na seriakli tawala. Katika suala hilo haki zao  muhimu pia  kama kupewa elimu na uduma ya afya bado hazijapatiwa ufumbuzi.  Masuala hayo yanatakiwa kugonga vichwa vya habari ulimwenguni kote  kupitia pia mashirikia ya kujitegemea ya kutetea haki za binadamu na mashirika ya kujitolea. Serikali ya Myanmar inatakiwa kutoa ufufunuzi kuhusu ukweli wa mabo katika eneohilo ambalo limekumbwa na mauaji na jeshi kuhusishwa. 

  4. Bangladesh inaitaji pia msaada.  Bangladesh kwa sasa ipo katika hali ambayo inaitaji msaada na jambo la kupokea jamii ya rohingya iliokimbia mauaji hali ya kutegemea msaada lazima itaongezeka. Nchini hiyo isiachwe pekee yake katika juhudi zake za kutoa msaada kwa wakimbizi kutoka Rakhine.  

  5. Mashirika kutoka nchini Uturuki kama AFAD ,Kızılay, TİKA , İHH na mashirika mengine ya kutoa misaada yamonesha ni kiasi gani kulikuwa na umuhimu wa kutoa msaada wa watu wenye kuhitaji msaada.

  6. Kundwa kwa tume ambayo itaongozwa na Uturuki kutatau mgogoro. 

  7. Suala la Rakhine sio suala mablo linahusi waislamu pekee bali linahusu ulimwengu mzima kama suala zima la Jerusalem. Kuna umuhimu mkubwa kuzungumzia suala hilo ili kitambulike kile ambacho kinaendelea . Mke wa rais wa Uturuki Bi Emine Erdoğan alietembelea kambi abazo walipokelwa wakimbizi hao na kushuhudia hali alisi  ya wakimbizi.   

     

Mara kadhaa mabadiliko hujitokeza na mambo mengi hubadilika. Mabadiliko ya hali ya hewa, inaweza kuwa katika Bahari ya Mediterania. Hivyo usisimami. Shirikiana na wenzako katika matatizo. Onyesha kama umechosha na udhalimu, kuwa na matumani na undoe khofu. Watoto na kizaki kipya knataraji kuwa na matumaini na maisha bora.

Kipindi chetu mmetaarishiwa kutoka chuo kikuu cha Yıldırım Beyazid katika kitivo cha Siasa na Profesa Dr. Kudret BÜLBÜL.                                                          Habari Zinazohusiana