"Brexit haitoathiri mahusiano ya kibiashara kati ya Uturuki na Uingereza"

Kujitoa kwa Uingereza Umoja wa Ulaya hakutakuwa na athari zozote za kibiashara kati ya Uturuki na Uingereza.

"Brexit haitoathiri mahusiano ya kibiashara kati ya Uturuki na Uingereza"

Kujitoa kwa Uingereza Umoja wa Ulaya hakutakuwa na athari zozote za kibiashara kati ya Uturuki na Uingereza.

Hayo ameyazungumza waziri wa uchumi wa Uturuki  Nihat Zeybekci wakati wa mkutano wake na waziri wa biashara za kimataifa wa Uingereza Liam Fox.

Kwa mujibu wa habari,mawaziri hao wamesema Brexit haitoathiri biashara kati ya Ankara na London.

Vilevile wameahidi kuwa hatua muhimu zitachukuliwa kuhakikisha uhusiano wa kiuchumi,bashara na uwekezaji unabaki palepale kama ilivyokuwa kabla ya Brexit.

Fox ameongeza kwa kusema Uingereza inataka kuendelea kuwa na mahusiano mazuri na Uturuki.Habari Zinazohusiana