Vita vya kimataifa vya uongozi Syria

Uchambuzi wa matukio kutoka kwa mtunzi na muandishi Can ACUN kutoka katika kitengo cha utafiti wa kisiasa, kiuchumi na jamii SETA

Vita vya kimataifa vya uongozi Syria

 Mapambano  ya kimataifa ya kupigania uongozi nchini Syria amepelekea vita  vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.  Kitendo cha rais wa Syria Bashar al Assad kutupilia mbali madai na maombi ya raia mwaka 2011 kimepelekea Syria  kutumbukia katika dimbwi la machafuko  kwa kuwa  hali hiyo imetoa fursa kwa mataifa  yenye ushawishi  katika ukanda kuingia pia katika mapambano ya kugombea utawala nchini Syria na kuwa na ushawishi zaidi.

Syria imekuwa ukumbi wa maipgano,  kwa upande mmoja kuwa uhalifu na mapigano yanayosababishwa na makundi ya kigaidi na upande mwingine  mzozo wa ndani.  Kwa upande mwingine vita baina ya mataifa yenye ushawishi nchini Syria na mataifa katika ukanda inaendelea. Mataifa ambayo yana ushawishi  nchini Syria kutoka na mzozo ambao unaendelea nchini humo ni pamoja na Urusi, Marekani, Uingereza, Ufaransa, Uturuki, Iran, Saudi Arabia, Qatar  na Israel.

Mataifa hayo katika mzozo wa Syria yanatumia ushawisha wao  ili kufikia katika malengo  yaliojiwekea  kuhusu Syria.

Urusi lkwa ushirikiano na Iran zinatoa usaidizi  kwa jeshi la anga na ardhi kwa jeshi la Syria na uongozi wa Assad.  Kwa upande mwingine jeshi la anga na ardhi la Urusi, wapiganaji wa kulipwa  kutoka Urusi wapo nchini Syria. Kwa upande wa Iran, inatoa usaidizi wa kifedha  na kijeshi pia ila inatoa pia mafunzo  kwa jeshi al aAssad. 

Kinyume na ilivyo Urusi, Iran ina wanamgambo wengi nchini Syria  wakiwemo pia  wageni miongoni mwaoa. Ina wanamgambo kama kundi la Hezbullah kutoka nchini Lebanon, kundi la Al Zaynabiyyun kutoka nchini Afghanistani, makundi mengine kutoka Irak kama al Nujaba  na mengine mengi.

Wanamgambo wengine wa kigenni nchini Syria, Iran ina  wanamagambo kutoka nchini humo ambao wamepewa jina la "walinzi wa raia".

Urusi na Iran zina kambi kadhaa nchini Syria  katika amaeneo tofauti na zinatumia viwanja vya ndege katika ameneo hayo.  Marekani, Ufaransa na Uingereza  nazo zimeunda  kundi la mapambano nchini Syria.   Mataifa hayo  yameona ni vema kwao kushirikiana na kundi la kigaidi linatambulika vema kuwa tawi la kundi la kigaidi la PKK. Kundi la YPG linatumiwa na mataifa hayo na kupewa msaada kwa kisingizio kuwa  lina mchango mkubwa katika mapambano dhidi ya kundi la kigaidi la Daesh. Kundi hilo linalindiwa usalama, YPG lipo katika eneo la  Manbij hadi Kaskazini-Magharibi kwa Syria ,  Abu Kamal hadi Kusini -Mashariki mwa  Syria.

Marekani na Ufaransa  zina zaidi ya kambi 25 za kijeshi  katika amaeneo hayo.  Marekani na Uingereza zinakambi mbili za jeshi katika eneo la Tanaf  Kuisini mw a Syria. Kambi hiz zimepewa jina la Magavir na al Savra. Licha ya kuwa  Saudi Arabia inaunga mkono upinzani Syria  na namna tofauti kwa kipindi cha muda kadhaa, kwa sasa inaonekana kuanza kunga mkono kundi la  demokrasia  ambalo pia linaonekana kuongozwa na kundi la wanamgambo wa YPG.

Kwa upande mwingine , mataifa ya kiarabu ambayo yanaongozwa na  Saudi Arabia  yameanza kuzungumzia  uwezekano wa kutuma wanajeshi  katika maeneo ambayo yanadhibitiwa na kikundi hicho.

Kwa uapnde wa Uturuki, inaunda eneo lingine .  Uturuki imeunda en eo la uchunguzi katika maeneo 9 Idlib , maeneo ambayo yaliundwa kwa lengo la kuchunguza utekelezwaji wa makubaliano ya kusitisha mapigano.  Uturuki inaenedelea kuwaweka wanajeshi wake  katika maeneo ambpo wanmagambo wa kundi la kigaidi la Daesh na YPG waliondolewa na jeshi la Uturuki katika operesheni ya Efratia na operesheni ya Tawi la Mzaituni.

Jeshi la Polisi la Syria ambalo lililpewa mafunzo na jeshi la Uturuki linalinda usalama Afrin baada ya magaidi kuondolewa katika eneo hilo pamoja na Azez na al Bab. Maeneo hayo yamekuwa salama na raia kuweza kuendesha maisha yao kama ilivyokuwa hapo awali.

Jeshi la polisi ambalo limepewa mafunzo n'a upi'nzani n'a ambalo wanamgambo ushirikiano n'a utawala wa mpito Syria. Jeshi la Syria Kwa upande serikalini. Qatar ulikuwa ikiunga mkono upi'nzani Ila baada ya mgogoro kuzuka,  ushawishi wake ulipungua Syria.

Mtendaji mwingine no Israel, Israel ilikalia kimabavu milima ya Golan katika vita vya mwaka 1967 . Israel ilikalia milima ya Golan ya Syria. Kitendo hicho no kinyume na makunaliano ya kimataifa. Kutokana na mzozo ulioibuka nchini Syria mwaka 2011, Israel imezidisha uwepo wake na kujidhatiti katika milima ya Golan.

Israel ikiwai Kuwa inakeraishwa  na uwepo wa Iran na  na wanamgambo wa kundi la Hezbollah kutoka Iran,jeshi la Israel huendesha mashambulizi ya anga mara Kwa  mara yakilenga ngome za Iran na Hezbollah Syria.Arshi ya Syria imekuwa ukumbi wa mapambano Kati ya Mataifa yenye ushawishi katika ukanda  na Mataifa yenye nguvu ulimwenguni tangu mwaka 2011 wakati rais Assad aligoma kusikia maombi na  matakwa ya raia.

Uchambuzi  wa matukio kutoka kwa mtunzi na muandishi  Can ACUN kutoka katika kitengo cha utafiti wa kisiasa, kiuchumi na jamii SETA

 

 Habari Zinazohusiana