Rais Erdoğan asema kuwa Uturuki itaendelea ushirikiano wake na Uingereza hata baada ya Brexit

Rais wa Uturuki Recep Tayyıp Erdoğan afahamisha Jumapiki kuwa Uturuki itaendela ushirikiano wake katika sekta ya na Uingereza hata baada ya Brexit

Rais Erdoğan asema kuwa Uturuki itaendelea ushirikiano wake na Uingereza hata baada ya Brexit

Rais wa Uturuki Recep Tayyıp Erdoğan asema kuwa Uturuki itaendelea ushirikiano wake katika sekta ya uchumi na Uingereza hata baada ya Brexit.

Brexit  ni pmpango wa Uingereza kujiondoa katika Umoja wa Ulaya.

Rais Erdoğan ameyazungumza hayo na waandishi wa habari muda mchache katika uwanja wa ndege wa Atatürk mjini Istanbul kabla ya kuanza safari yake kuelekea nchini Uingereza ambapo anataraji kukutana na waziri mkuu wa Uingereza Theresa May.

Ziara hiyo ya rais wa Uturuki itachukuwa muda wa siku 3.

Rais Erdoğan amewaambia waandishi wa habari kuwa  atazungumza na waziri mkuu wa Uingereza Bi Tehersa May kuhusu ushirikiano katika mapambano dhidi ya ugaidi na ushirikiano katika juhudi za kutatua mizozo katika ukanda.

 Habari Zinazohusiana