Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki Mevlüt Cavusoglu kukutana na Mike Pompeo Juni 4
Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki Mevlüt Cavusoglu kukutana na Mike Pompeo mjini Washington ifikapo Juni 4

Waziri wa mambo ou nje wa Uturuki Mevlüt Cavusoglu atarajiwa kukutana na Mike Pompeo ifikapo Juni 4 mwaka 2018.
Viongozi hao wa kidiplomasia wa Uturuki na Marekani watakutana mjini Washington kama ilivyofahamishwa na vyanzo vya habari katika ofisi za viongozi hao.
Kutokana na muda kuwa mchache , viongozi hao ilikuwa wakutane Mei ila wameafikiana kuwa watakutana ifikapo Juni 4 mjini Washington.
Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki Mevlüt Çavuşoğlu katika ziara yake hiyo mjini Washington atazungumzia ushirikiano katika mapambano na kundi la kigaidi la PKK, PYD/FETÖ na hali inayoendelea katika eneo zima la Mashariki ya Kati.
Pompeo na Çavuşoğlu walikutana na kuzungumza mjini Brusssels katika mkutano wa NATO Aprili 27 mwaka 2018.