Uchambuzi wa Matukio, matukio muhimu mawili mashariki ya Kati

Matukio muhimu mawili Mashariki ya Kati, uchagzui nchini Iran na uhamisho wa ubalozi wa Marekani mjini Yerusalemu, Utafiti kutoka katika kitengoc ha SETA na Can Acun

Uchambuzi wa Matukio, matukio muhimu mawili mashariki ya Kati

Mtukio muhimu mawili Mashariki ya Kati ni pamoja na uchaguzi uliofanyika nchini Iran ikiwemo pia uhamisho wa ubalozi wa Marekani kutoka mjini Tel Aviv na kuhamishwa mjini Yerusalemu. Tathmini ya kpindi chetu imetaarishwa na Can Acun kutoka katika kitengo cha  utafiti wa kisiasa, uchumi na jamii SETA.

Ulimwengu mzima ulisimama kidete baada ya rrrais wa Marekani Donald Trump kutanga rasmi kuwa serikali yake inatambua mji wa Yerusalamu kama mji mkuu wa Israel na kufahamisha kuwa  ubalozi wake ulioko mjini Tel Aviv utahamishiwa mjini Yerusalemu bila ya kujali makubaliano ya kimataifa.

Ikıwa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limepinga uamuzi wa Marekani kuhamisha ubalozi wake, katika kura iliopigwa kuhusu Yerusalemu Marekani iliweka kura yake ya turufu kwa lengo la kuzuia  msuada wa sheria wa Umoja wa Mataifa.  Pendekezo la wanachama wa Umoja wa Mataifa lilichanguliwa na karibu wanachama wote  kwa kuonesha msiamamo ambao ulipinga uamuzi wa Marekani kuhusu Yerusalemu.

Muungano wa mtaifa ya kiislamu ulikutana kufuatia wito uliotolewa na rais wa Uturuki Recep Tayyıp Erdoğan . Mataifa ya muungano huo yalikemea kwa tamko la pamoja uamuz wa Marekani  uliotolewa na rais Donld Trump kuhusu Yerusalemu.

Kama ilivyokawaida kutokana na kura ya turufu, licha ya uamuzi huo wa Marekani kupingwa na kiasi kikubwa cha mataifa wanachama wa Umoja wa Mataifa, Marekani imehamisha ubalozi wake Yerusalemu. Rais wa Uturuki Recep Tayyığ Erdoğan mara kwa mara huzungumzia kuwa mataifa matano sio makubwa kuliko ulimwenguni mzima akilenga mataifa wanachawa wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa ambayo huchukuwa uamuzi wa kupitisha au kuzuia  misuada na mapendekezo ambayohutolewa.

Baada ya matukio yote hayo rais wa Marekani Donald Trump hakuweza kuachakile ambacho alikuwa tayari ameamua. Rais wa Marekani alionesha kuwa ataendelea na msimamo wake ambao unashinikizwa na "wahayi" wa  kanisa na viongozi wanaodai kuwa Yerusalemu ni mjini mkuu wa kiyahudi.  Kuhani alieshiriki katika ufunguzi wa ubalozi wa Marekani Yerusalemu anatambulika ka misimamo yake mikali. Wkati huo huo ni kwamba siku kadhaa zilizopita wapalestina walikuwa wakiandamana kupinga kuzuliwa kwao kurejea katika makaazi yao. Binti wa rşa wa Marekani Donald Trump, Ivanka Trump akishirikiana na mumewe walijiekeza Tel Aviv na baadae mjini Yerusalemu.  Wpalestina walikuwa wakiandamana kupinga kuzuliwa kwao kurejea katika mkaazi yao. 

Maandamano makubwa yalifanyika Ukanza wa Gaza katika mpaka wa Israel na eneoı hilo la wapalestina.

Wapalestina wanaoishi Ukanda wa Gaza kama wapo katika gereza la wazi kutokana na matendo ya kinyama wanaotendewa na jeshi la Israel. Katika maandamano Ukanda wa Gaza jeshi la Israel limetumia silaha za moto kuwatwanya waandamanai na kusababisha vifo vya wapalestina waliokuwa wakiandamana kwa amani kuuawa na wengine zaidi ya 2 770 kujeruhiwa. 

Wakati ambapo wapelestina wakiuawa, mkwe wa Trump na bnti yake  walikuwa katika hafla ya ufunguzi wa ubalozi wa Marekani Yerusalemu na kusherehekea kufunguliwa kwa ubalozi wa Marekani.  Licha picha na video zilizonaswa na kupeperushwa na vyombo vya habari kuhusu unyanyasaji wa jeshi la Israel, Marekani inatuhumu chama cha Hamas  kuwa sababu ya ghasia katika maeneo ya wapalestina. Niwa zi kuwa Marekani haijali uhalifu ambao unatendwa na jeshi la Israel. Moja wa sababu ambazo zinaifanya Marekani kutokujali hali ya Palestina na wapalestina ni ushirikinao wa baadhi ya mataifa ya kiarabu na Marekani. Baadhi ya mataifa ya kiarabu  yanamuunga mkono rais wa Marekani Donald Trump. Ni wazi kuwa Uturuki ndio taifa pekee ambalo linajitolea kwa kiasi kikubwa kutetea haki wa wapalestina.  Mtaifa maengine ya kiarabu yanafumbia maho suala hilo kwa kuwa Marekani nalinda usalama wa utawala wa baadhi ya mataifa hayo ya kiarabu kuendelea kuwa madarakani.  Uturuki pekee ndia taifa ambalo limetangaza siku tatau za maombolezo kutoka na maafa ya wapalestina waliouawa na jeshi la Israel katika maandamano Ukanda wa Gaza na kukemea wazi unyanyasaji wa jeshi la Israel . Bunge la Uturuki limekemea pia mwenendo wa Israel dhidi ya wapalestina.

Uturuki ilimtaka balozi wa Israeli kuondoka Uturuki na kumuamuru balozi wake kurejea nchini Uturuki kutokana na hali iliko Ukanda wa Gaza na maeneo  ya wapalestina.

Jambo jingine ambalo lilikuwa muhimu Mashariki ya Kati ni uchuguzi wa wabunge nchini Irak.  Uchaguzi Irak ulikuwa na umuhimu mkubwa pia kutokana na mapambano dhidi ya wanamgambo wa kundi la Daesh, mji wa Mosul na miji mingine ka Faluja na Anbar kutokana na mapigano ya yaliibuka  na kuchukuliwa na uongozi wa  Irak. Miji iliokuwa na utata kwama  Kirkuk na Sinjar  ilikuwa na lengo la kutaka kujitengo na kura ya maoni iliandaliwa. watu walioshiriki katika kura hiyo ni asilimia 44.

Kulikuepo na orodha  akiwemo  waziri mkuu wa Irak Haidar al Abadi, waziri mkuu wa zamani Nuri al Maliki, kiongozi wa dhehebu la shia Muktada al Sadr na Hashd al Shaabi.

Kulikuepo poa muungano baina kiongozi Usama Al Nijaifi, kiongozi wa dhehebu la Shia Ammar Al Hakim. Wakati  huo huo muungano baina ya waziri wa.zamani wa Irak Nuri alMaliki na orodha ya Fatah ya Hashd Al Shaabi , muungano huo umechukuliwa Kuwa na ukaribu na Iran. Haidar Al Abadi n'a Moktada Sadr wan ushirikiano na Marekani na Saudi Arabia.

Kulingana  na taarifa zizlitolewa na kamati iliosimamia uchaguzi nchini Irak,  orodha ya Al Sadr  imeoneshwa kuwa kama ndio imeshinda katika uchaguzi huo. Nafasi ya pili  ni ya Hashd a Shaabi,  waziri  mkuu wa zamani wa Irak al Abadi  alichukuwa nafasi ya tatu , Nuri al Maliki nafasi ya  nne.  Ushawishi wa Iran  unatakiwa kupunguka baada ya uchaguzi.

Orodha ya waziri mkuu wa zamani Nuri al Maliki haitakiwi na kundi la Hashd al Shhabi halitakiwi kushiriki katika serikali.

Hata kama Iran itapunguza ushawishi wake Irak, itaendelea kuwa  mtendaji muhimu katika siasa za Irak. Hashd al Shaabi kuwa nafasi ya pili  kwa ushawishi baada ya jeshi la Irak, inaweza kuwa ikiongozwa chini ya umiliki wa  Iran.

Wakati wa matokeo ya uchaguzi Irak, kulitakiwa  kuwa siasa za nchi hiyo ziwe  chini ya ushawishi wa Saudi Arabaia na Marekani. Siasa hizo ziwe  na ushawishi wa mataifa hayo mawili Mashariki ya Kati.  Kiongozi wa dhehebu la kishia Moktada al Sadr alikuwa akiongoza kundi ambalo lililkuwa likikabilaina na Marekani miaka kadhaa iliopita. Kundi hilo lililokuwa likiongozwa na al Sadr kwas asa limeonekana kuwa  na ushirikiano mzuru na Marekani na Suadi Arabia. Wakati huo huo, waziri mkuu wa Irak Haidar al Abadi aliwekwa katika uongozi baada ya Mosul  kukombolewa kutoka mikononi mwa Daesh na Marekani. 

Abadi alifanya ziara  nchini Saudi Arabia na alikuwa tayarai kushirikiana na Marekani na Suadi Arabia. Hali hiyo ilichukuliwa ili kuzuia ushawishi wa Iran.

Licha ya kuwa uchaguzi Irak ulikuwa na vipengele muhimu kwa Uturuki, mapambano dhidi ya ugaidi yalikuwa na umuhimu mkubwa kwa usalama wa Uturuki.  Operesheni dhidi ya ugaidi zilizoendeshwa  mpakani mwa Irak Kaskazini, jeshi la Uturuki lililenga  kundi la kigaidi la PKK. Operesheni ya kijeshi la Irak  kwa ushirikiano  na jeshi la  Uturuki  ina umuhimu mkubwa katika ushirikiano. 

 

Matukio muhimu mawili Mashariki ya Kati, uchagzui nchini Iran na uhamisho wa ubalozi wa Marekani mjini Yerusalemu, Utafiti kutoka katika kitengoc ha SETA na Can Acun

 

 

 

 Habari Zinazohusiana