Trump amrushia maneno makali mwigizaji wa Hollywood Robert De Niro

Rais wa Marekani Donald Trump amemjibu mwigizaji wa Marekani Robert De Niro kwa kumrushia maneno makali.

Trump amrushia maneno makali mwigizaji wa Hollywood Robert De Niro

Rais wa Marekani Donald Trump amemjibu mwigizaji wa Marekani Robert De Niro kwa kumrushia maneno makali.

Mwigizaji huyo alimkashifu Trump katika tuzo za Tony siku moja iliyopita.

Trump naye ameamua kumshambulia mwigizaji huyo kupitia ukurasa wake wa Twitter wakati akirudi kutoka Singapore.

"Robert De Niro, ambaye ana IQ ya chini sana, amekuwa akipigwa ngumi za kichwa na wanandondi wa ukweli katika filamu zake na hivyo basi nadhani amepoteza uwezo wake wa kufikiri",alisema Trump.

"Sidhani kama anajua  kuwa uchumi wetu ni bora zaidi kwa sasa na kwamba makampuni mengi yameibuka." aliongeza Trump.

Katika tuzo za 72 za Tony, Robert De Niro aliimba wimbo wa kumkashifu rais wa Marekani Donald Trump.

Watazamaji waliupokea wimbo huo kwa shangwe.

 Habari Zinazohusiana