Uturuki yapongeza maafikiano baina ya Marekani na Korea Kaskazini

Serikali ya Uturuki yapongeza maafikiano baina ya rais wa Marekani Donald Trump na rais wa Korea Kaskazini Kim Jong Un

Uturuki yapongeza maafikiano baina ya Marekani na Korea Kaskazini

 

Serikali ya Uturuki imepongeza  maafikinao yalioafikiwa baina ya rais  wa Marekani   Donald Trump  na rais wa Korea Kaskazini Kim Jong Un mwanzoni mwa juma .

Uturuki imepongeza hatua iliopigwa baina ya Korea Kaskazini na Marekani kwa lengo la kudumisha amani katika  Ghuba ya Korea.

Tangazo la kupongeza  hatua hiyo limetolewa na wizara ya mambo ya nje  ya Uturuki Jumanne.  Mkutano baina ya rais wa Marekani Donald Trump na rais wa Korea Kaskazini Kim Jong Un ulifanyika Juni 12 nchini Singapore.

Tangazpo hilo la wizara ya mambo ya nje ya Uturuki limepongeza  hatua hiyo yenye lengo la kudumisha amani katika  ukanda.

Uturuki itaendelea kuunga mkono  juhudi za kudumisha amani   katika ghuba ya Korea.

 

 Habari Zinazohusiana