Venezuela kusafisha dhahabu yake nchini Uturuki

Waziri anaehusika na uchimbaji wa madini Venezuela amesema kuwa dhahabu yake itakuwa ikisafishwa nchini Uturuki

Venezuela  kusafisha dhahabu yake nchini Uturuki

 

Waziri anaehusika na uchimbaji wa madini nchini Venezuela amesema kuwa Venezuela itakuwa ikisafisha dhahabu yake nchini Uturuki badala ya  Uswisi.

Taarifa hiyo kuhusu Venezuela kusafisha  dhahabu yake nchini Uturuki imefahamishwa na waziri anaehusika na madini Victor Cano.  Venezuela imechukuwa uamuzi kutokana na  vikwazo iliowekewa.

Katika mkutano na waandishi wa habari Victor Cano amesema kuwa makubalaino  na Uturuki kati ya benki kuu ya Uturuki na Venezuela  tayari yamekwisha sainiwa.

Hapo awali Venezuela ilikuwa ikisafishia dhahabu yake nchini Uswisi na kuchukuwa uamuzi wa kusafisha dhhabu yake Uturuki kutokana vikwazo iliowekewa. Uturuki na Venezuela ni mataifa washirika.

 

 Habari Zinazohusiana