Ni wapi Syria inakoelekea ?

Kutoka katika chuo kikuu cha Ankara Yildirim Beyazit katika kitengo cha siasa Dakatari  Kudret BÜLBÜL  anatufafanullia

Ni wapi Syria inakoelekea ?

Vita nchini  Syria vimekwisha ingia katika mwaka wake wa 7 tangu kuanza kwake.  Ni unyama mkubwa umetendwa nchini humo ambapo watu wasiokuwa na atia wamepoteza maisha.  

Mazungumzo ya amnai kwa ajili ya Syria yaliofanyika mjini Astana  na kusitishwa kwa mapigano Idlib ndio mada kuu ambazo zinazungumzwa katika vyombo vya  habari ulimwenguni. 

Vile vile kunazungumziwa kuhusu mashambulizi  ya jeshi la Urusi katika maeneo tofauti nchini Syria. Mamilioni ya  raia wa Syria wamelazimika kuondoka katika makaazi yao wakihofia mapigano na mashambulizi.

Mashambulizi ambayo yametekelezwa nchini Syria, silaha za kemikali zimetumiwa kama ripoti za uchunguzi zinavyofahamisha. Hali ya  mauaji na unyama  ncchini humo ni kama  filamu za kutisha.

 

Kutoka katika chuo kikuu cha Ankara Yildirim Beyazit katika kitengo cha siasa Dakatari  Kudret BÜLBÜL  anatufafanullia mada yetu…

Katika juhudi za kurejesha amnai nchini Syria, Uturuki, Iran na Urusi zimekutana kuzungumzia hali inayoendelea nchini humo. Mkutano huo kati ya mataifa hayo matatu umefanyika Juma lililopita mjini Tehran nchini Iran.  Kulizungumziwa  kuhusu hali halisi mjini Idlib .

Ulimwengu wa Magharibi uliwekwa kando. Uturuki imekemea ukimya wa umuiya ya kimataifa na mashirika  ya kimataifa. Jumuiya ya kimataifa inaonekana kufumbia macho  unyama na ukatili unatendwa nchini humo.

 Mkutano uliofanyika Tehran  kuhusu Syria ulioneshwa moja kwa moja ili mtu yeyote kuelewa ni kipi kilichoendelea katika mazungumzo hayo.

Katika mazungumzo hakuna kiongozi ambae alionekana kusikitishwa na  madhila yanayowakumba  raia wa Syria.

Rais wa Uturuki Recep Tayyıp Erdoğan amekuwa mara kwa mara  akitolea wito wa kusitishwa mapigano .  Ifahamike kuwa Uturuki imewapokea wakimbizi zaidi ya milioni 4,5 wakiwemo wakimbizi kutoka Syria.

Uturuki ni taifa ambalo lipo mtari wa kwanza  kuathirika na mgogoro wowote ambao utatokea katika mataifa jirani. Wajibu wake ni pamoa na kutoa huduma ya kwanza kwa waathirika.

Maelefu ya wakimbizi na wahamiaji wameolewa  upande  uliojificha wa  Umoja wa Ulaya, «  haki sawa, uhuru na udungu » ni maneno tu ambayo hayakutani na vitendo, wakimbizi na wahamiaji  wjipata wakitumiwa tu  moja ya   vyanzo vya nguvu kati. 

Uturuki  kwa upande wake inaonekana kutimiza wajibu wake wa  kihistoria  kama inavyofahamika  kwa kutoa misaada ya kibinadamu. Uturuki haijachoko kutoa msaada kwa wakimbizi licha ya vita kudumu kwa zaidi ya miaka 6 sasa.

Urusi bado inaendelea kuunga mkono serikali ya Syria na kuwa na ushawishi katika eneo la Mediterania na sio kama ilivyokuwa ikidhaniwa Krimea, Georgia na Ukraina. Urusi sasa imekuwa na ngome zake nchini Syria. Urusi nchini Syria ni eneo ambalo lipo mbali na ulimwengu wa Magharibi.

Iran nayo inaendelea na ushawishi wake kwa upande mwingine nchini Syria. Ali Riza Zakani  ni mmoja miongoni mwa wabunge  ambao humzungumzia kiongozi wa imani Ali Khamenei. Ali Riza amesema  mataifa matatu ya kiarabu ni mataifa ya  muamko na mabadiliko ya kiislamu.

Matamshi yaliotumiwa katika  nyaraka tofauti yameonesha kwamba mji wa nne kaiarabu   umeingia na vuguvugu la mabadiliko. Mji mkuu wa Syria umekuwa kama mji mkuu wa Lebenon, Irak na Yemen amesema Zakani na kushangazwa vipi  Iran imeweza kujipenyeza. Ila baadhi ya wakaazi katika  maeneo hayo wanatambua kwamba  Iran pia inachanangia damu kumwagika.  Mji mkubwa nchini Irak ukiwa mji wa pili nchini humo ni mji wa Basorah, mji ambao una bandari  muhimu miongoni mwa bandari muhimu katika eneo hilo. Wakaazi wengi Basorah ni waumini wa dhehebu la shia.

Haukana mkimbizi hata mmoja ambae alijaribu kukimbilia nchini Iran kutokana na kwamba katika maandamano  ublaozi mdogo wa nchi hiyo nchini Irak Irak ulishambuliwa na waandamanaji.

Taifa ambalo pia linastahili kuzungumziwa katika mzozo wa Syria ni Israel, tangu kuundwa kwake Israel imekuwa ikiendesha siasa zake ambazo  malengo yake pia ni kuwa na ushawishi katika ukanda kwa kutoa msaada wa upinazani ni kujaribu kuwaondoa  katika uongozi wale ambao wanapinga mwenendo wake katika ukanda.

Siasa za Israel katika  katika uapnde wa kizayuni  ni kwamba eneo ambalo lipo kusini mwa Uturuki ni « nchi y ahadi » hadi kupelekea kuandwa kwa mkakati wa Israel yenye nguvu.Tangu mwanzo  muelekeo wa kisiasa ulikuwa  ukielekea katika   mtazamo huo. Marekani hairidhishwi na utawala uliopo nchini Syria.

Marekani imetoa usaidizi wa silaha na mafunzo kwa kundi la wanamgambo wa PKK na tawi lake la PYD. Marekani imefahamisha ywa kwamba kufanya hivyo ni kwa lengo la kukabiliana kundi la kigaidi la wanamgambo wa Daesh.  Kwa upande mmoja au mwingine  uamuzi huo ulichukuliwa kwa ajili ya  kuzuia  kujipenyeza kwa Iran.

Marekani imefahamisha kuwa inakata misaada yake kwa mataifa mabyo hayafuati mapendekezo yanaotolewa na Marekani. 

Marekani ina unga mkono mwenendo wa Israel wa kuendelea na ujenzi katika maeneo ya wapalestina yaliokapiwa kimabavu.  Urusi nayo kwa upande wake  ina unga mkono  serikali ya Syria. Wakati huo huo jumuiya ya kimataifa ikiitaka serikali ya Syria kusitisha mashambulizi yake.

Umoja wa Ulaya bado wanajadili hatma ya wakimbizi  kutoka Syria nchini Uturuki. Wakimbizi ambao  baadhi yao  wanaonekena kuanza kurejea katika taifa lao kuliko  kubaki ugenini.-

Viya vya Syria na uhalifu wake vinashuhudiwa  na ulimwengu mzima.  Hali ambayo naendelea katika ardhi ya Syria kwa kwel sio hali ya kuridhisga.  Jamii tofauti nchini humo kwas asa vile vile zinaonekana kutenganishwa ili kufikia malengo yaliowekwa kwa ajili ya kuitawa Syria.

Kuna pande tofauti zinzohasimaina. Upande mmoja serikali huku upande mwingine ukiwa ni  wapinzani vile vile hatuwezi kuweka kando ushawishi wa  Magharibi.

Magharibi huwa ikifahamisha kuwa nchini Syria kuna vitovu  na maficho ya magaidi. Uruısi nayo kwa upande wake huwa ikifikia hatua ya kushambulia kwa mabomu maeneo hayo bila ya kujali raia wanaoishi katika maeneo hayo.

Maelefu ya wakaazi wamejipata katika hali mbaya ya umaskini na kulazimika kuhama na kukimbia nchi. Je mnadhani kuwa watu zaidi ya milioni wanaweza kuwa magaidi ? taunatakiwa kujiuliza swali. Malengo sio kutawanya  jamii katika eneo hilo. Kunaonekana kuwa maşengo yake ni kulikgawa eneo hilo kijiografia kwa kuweka miji tofauti. Je ?  kuna mapambano thabiti ya dhidi ya makundi ya kigaidi kwa ushirikiano na wakaazi wanaoshi katika maeneo ambayo kunadhaniwa kuwa na magaidi ? raia wasiokuwa na hataia pia wamekuwa  katika mateso kwa muda mrefu.

Ni vipi atatofautishwa raia wa kawaida na gaidi anaieshiriki katika makundi ya wapiganaji ? Uturuki hgaina haja ya kulipwaa kwa kile inachojitolea nchini Syria bali  ubinadamu na kiwi cha amani katika ukanda.  Vita vya Syria ni viti visivyokuwa na malengo kwa faidi ya Syria na raia wake.

Vita hivyo vinatkiwa kukomeshwa, na iwapo hakutochukuliwa hatua  basi itakuwa vigumu kufikia katika  hali inayotarajiwa.  Watoto  na wanawake wanauawa bila ya hatia yeyote, silaha za kemikali. Tukirudi nyuma tunakumbuka kifo vcha Ayan ambae alizama baharini  wakati wakikimbia mapigano na mabamu ya kemikali  .

Tunakumbuka katika historia katika kpindi cha uongozi wa Idi Amin,  Staline, Pol Pot, Hits, Musolini, Yvan  Robespierre , Dracula (Voyvoda) na vipongozi wengine ambao wanafahamika kwa kile ambacho walitenda katika historia ulimwenguni. Licha ya uavu kuchukuwa muda,  haki hutendekea.

 

Kutoka katika chuo kikuu cha Ankara Yildirim Beyazit katika kitengo cha siasa Dakatari  Kudret BÜLBÜL  ametufafanulia

 Habari Zinazohusiana