Umoja wa Ulaya wapitisha marekebisho katika sheria kukabiliana na utakatishaji pesa

Nchi za umoja wa ulaya zimepitisha kanuni mpya kukabiliana na utakatıshaji wa pesa kwa ufanisi zaidi

Umoja wa Ulaya wapitisha marekebisho katika sheria kukabiliana  na utakatishaji pesa

Nchi za umoja wa ulaya zimepitisha kanuni mpya kukabiliana na utakatıshaji wa pesa kwa ufanisi zaidi

Wajumbe kutoka wizara husika za nchi 28 za umoja wa ulaya wamekutana jıjıni Luksemburg katika kikao cha baraza la  haki na mabo ya ndani.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na baraza hilo la umoja wa ulaya wamekubaliana kupitisha miongozo mipya kukabiliana na suala la utakatishaji pesa.

Ufafanuzi mpya kuhusu utakatishaji pesa umetolewa pamoja na kuleta miongozo mipya inayohusu  adhabu kwa wale watakaokutwa na aina hii ya makosa ıkıwa pamoja na kuhakikisha watu hawa hawazipati tena mali zao zinazohusishwa na utakatishaji pesa.

Yeyote atakayekutwa na hatia atapewa adhabu ya kifungo mpaka maiaka minne na hakimu anaweza kumuongezea adhabu ya kulipa kama atavyoona inafaa, na wale ambao utakatishaji wa pesa unahusiana na makundi ya kigaidi adhabu itakuwa kali zaidi

Miongozo hii mipya pia itawezesha ushirikiano kati ya polisi na mahakama za nchi tofauti kushirikiana kirahisi kuhusiana na kesi hizi

Marekebisho hayo  miezi 24 baada ya kuchapishwa katika gazeti rasmi la umoja wa Ulaya yataingizwa pia katika sheriaza ndani za kila nchi mwanachama na kuanza kutumika.Habari Zinazohusiana